RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.09.2016: MCH. NOAH LUKUMAY: USIJITAMKIE MANENO YA KUSHINDWA, JITAMKIE USHINDI NA USIKATISHWE TAMAA NA MANENO YA WATU

Unaweza ukawa unatembea kwenye shida, mateso, hali ngumu usikate tama safari yako bado ni ndefu. Usiungane na watu walioshindwa hata kama umelala chini na wewe usiseme na mimi na lala chini na nimekwisha, ila sema, umelala kwa muda tu lakini baada ya muda utasimama tena.

Ili uweze kuishinda roho ya kukatisha tamaa unatakiwa kuona yale yasiyoonekana kana kwamba yanaonekana kwa IMANI. Watu wanaweza kukuuliza, “hivi mpaka leo hujazaa?” Mwambie, “bado sijazaa kwa sababu mtoto ninaye mbeba siyo wa kawaida ni mtoto wa miaka mikubwa, ni mtoto wa miujiza mikubwa”, watasema, “hadi leo hujaolewa?” Wambie, “mume wangu hafanani na wanaume wengine ninamngoja, anaandaliwa ninamngoja anatokea”, watakuuliza, “mbona mpaka leo hujafika mahali wenzako wafika?” wambie, “safari yao siyo yangu kama wamefika waningoje huko huko maana na mimi ninaelekea kule kule”.


Mch. Noah Lukumay

Ishinde roho ya kukata tamaa kwa kuona yale mambo yasiyoonekana kanakwamba yanaonekana, hata kama watoto wanavuta bangi au sigara au madawa ya kulevya, wanakunywa pombe, usikate tamaa kwa kuwa wanakunywa pombe leo lakini jua kesho inakuja hawa hawa walevi watakuwa waimba kwaya, watakuwa wanamwabudu Bwana watakuwa ni watu wa kumtumikia Mungu. Maandiko yanasema, “sisi hatuishi kwa yale yanayoonekana bali kwa yale yasiyoonekana”. Watu wa Mungu ni kama upepo unaovuma huwezi kutafuta upepo unaelekea wapi lakini kazi yake utaiona kule mbele.

Mungu akubariki sana kwa kusoma ujumbe huu na tunakukaribisha sana katika ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi mpaka saa 8 mchana Mlima wa Moto Mikocheni "B" na siku ya Jumatano katika ibada ya KUFUNGULIWA KWAKO saa 9 mchana hadi usiku

Haya ni mafundisho aliyofundisha Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili 25.09.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"