RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCH. OTIENO WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AFUNDISHA JUU YA MAISHA YA IMANI SIKU YA JUMAPILI 25.09.2016 KATIKA KIPINDI CHA SUNDAY SCHOOL


1. IMANI katika maisha yetu tunayoishi jambo la kwanza ni familiya, familiya ambayo inaishi pasipo imani ni rahisi kualawala. Hiyo biashara unayofanya usipo kuwa na imani nayo, usipo itiisha utakuta kuna wakati biashara inageuka inakuwa chungu kama hauna imani unaweza sema nimelogwa au nini?. Kwa kila jambo unalofanya ni lazima uwe na imani nalo kuwa litafanikiwa. Usiwe mtu wa kukata tama na kukosa imani ya kile unachofanya.

Mch. Otieno

2. NDOA 
Sasa hivi ndoa zinaharibika kwa sababu ya kutokuwa na imani, kutokuminiana mwingine kwa mwingine. Ni gharama gani uliyoichukua wewe uliyeko kwenye ndoa? Je, unamtii mume wako? na unaimani na mume wako na unamsikia? Sasabu Mungu anasema katika kitabu cha Isaya 54:4 “Usiogope, maana hutatahayarika wala usifadhaike maana hutaaibishwa kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.”

Mch. Francis Machichi (Kulia) Mch. Mama Mgetha

Wajane wanamsikiliza Mungu kwa sababu Mungu ndio mume wao, Je, wewe uliye na mume unamsikiliza, unamtii? Ndoa zinaharibika kwa sababu utii haupo kwenye ndoa? Ndoa zinaharibika kwa sababu Imani imetoweka, ndoa zinaharibika kwa sababu upendo haupo tena lazima tufufue Imani na Upendo uliokosekana ili urudi tena kwenye ndoa zetu ili tuweze kusimama. Ndoa inapoyumba na kanisa ni rahisi kuyumba.
3. MAGONJWA 
Sasa hivi yanatokea magonjwa ya kila aina magonjwa ambayo pengine hata daktari anashindwa kuyatibu. Tupo kwenye “super market” ya mbinguni ambako kila kitu tunapokea kwa Imani. Vitu ambavyo vinajitokeza kama vile magonjwa yanayo sababisha familia kuharibika, magonjwa, ndoa kuharibika, biashara kuaharibika na mambo mengi kuharibika kutokana na wewe kujikuta umekosa Imani kuwa Mungu anaponya magonjwa sugu, matokeo yake unajikuta ukitumia pesa nyingi unatumia kutibu ugonjwa wako. Lazima tuwe na Imani na utiifu ili tuweze kuvuka hapa tulipo. Kama huna Imani ni rahisi mtu kukudanganywa na kuambiwa huu ugonjwa wako tiba inapatikana na wewe unaenda huko na wanakutoza fedha nyingi.


Katika Biblia kuna yule mwanamke aliyevuja damu kwa miaka 12 Yesu alikuwepo lakini yalipomshinda ndipo aliamuwa kwenda kwa Yesu, yalipo kuwa yameoza yameharibika ikabidi aingie kinyume hakuweza kuingilia mbele alifanya maamuzi moyoni. Kuna maamuzi ambayo ukifanya kwa Imani Mungu anafanya. Yule mwanamke akasema, “Nikigusa pindo la vazi lake tu shida yake itakuwa imeisha”, vivyo hata leo ukifanya maamuzi ukisema nitakapo muona mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kanisani akiwa akisimama madhabahuni, “nikigusa hata miguu yake tu naamini nitapona”. Kwa imani hiyo Mungu atakuponya. Unatakiwa kuwa na Imani ya kutiishwa. 
4. KAZI Kazi za watu zimeharibika ofisini. Pengine unatamani kuacha kazi, uikimbie ofisi. Kwa Imani una mamlaka ya kuitiisha hiyo ofisi ili iweze kukusikiliza, una mamlaka ya kuitiisha hapo unapo fanyia kazi ukisema, “Kila kilicho inuka, nakitiisha na lazima baraka zitatokee ofisini kwangu na ninapo fanyia kazi.” Mtu mwenye Imani hakimbii maovu wala shetani. Shetani yupo popote unako kwenda, unachohitajika ni kuwa na Imani. Lazima tuwe na Imani kwani bila Imani ni kazi bure. Sasa hivi kunashida kwa sababu imani imetoweka, ndoa zinashida.

Kitabu cha Yohana 15:10 kinasema, “Mkisikiliza amri zangu mtakaa katika pendo langu kama vile mimi nilivyozishika amri za baba yangu na kukaa katika pendo lake.” Imani pia inahusiana na amri uliyopewa. Bwana ametupa tuwe na upendo lakini hivi sasa upendo umepotea, badala ya kupendana tunapigana vikumbo, yaani huwezi kupita vizuri mbele yangu na nilichokukosea sijui, watu wamekuwa na wivu? Hunipendi mimi na hata suti niliyoivaa ikiwa nzuri namna gani huipendi. Ukiona mwenzako amepita amependeza unaanza kusema, “mmh si vya wizi tu hivyo”. Na Bwana anatuambia tuwe na upendo. Yesu anawambia watu, “watafahamu kwamba nyie ni wanafunzi wangu kutokana na upendo mtakao kuwa mmependana.” Upendo ni nguvu, upendo unatuunganisha katika uwepo wa Mungu. Ukinipenda huwezi ukanisema vibaya bali utanisaidia. Yakobo anasema, “mhesabu ndugu yako ndio kioo chako”, mimi siwezi kuona mgongoni kwangu lakini wewe unaweza kuniona, sasa kama unanipenda hautaweza kwenda kutangaza huko alafu ukarudi kwangu na kuanza kusema, “tulijua tu huwezi kufika, tulijua tu kama hiyo ndoa haitakaa sana”, kama ulijua kwa nini usije kunisaidia?


JINSI TUNAMVYOMFAHAMU BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE Ukisoma katika kitabu cha Yohana 15:14 kinasema, Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Kwanini tumekuwa rafiki wa Yesu? Tunatenda aliyotuamuru Yesu tutende. Jumapili iliyopita niliwambia, Askofu wetu kanisa hili Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amekuwa na kanisa lenye akibari kwa sababu ya upendo alionao ndani yake, ni Askofu mwenye upendo, asiye na majivuno, Mungu amembariki, mnyenyekevu, anakubali kusalimia mtu yoyote, unamuona bila “appointment”, ni Askofu ambaye tukiita maombi ya kufunga anaingia na yeye kwenye maombi hayo ya kufunga lakini mwingine hawezi, ananyenyekea mbele zetu (Je, sisi ni akina nani?”).

Tunahitaji kumuombea, umkumbuke katika maombi yako ya kila siku. Askofu huyu ana upendo uliyopo ndani yake. Upendo hauhesabu mabaya, upendo hauna kiburi, upendo husitili. Tufunikane, tusiongee mambo yasiyofaa tukaliacha kanisa la Mlima wa Moto Tanzania uchi na tukiliacha uchi kanisa, inaonesha sisi bado tu watoto wadogo tunahitaji kukua kiroho. Tusome Waebrania 5:8-9, “Na ingawa ni mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata, naye alipokwisha kukamilishwa akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.”

Yesu aliyekuokoa alijifunza kutii na akawe sababisho la kukuokoa. Siku ya leo ukiwa na utii utawavuta watu wengi kwa Bwana, utawaleta watu wengi Mlima wa Moto, ili wapate kubadilishwa, watu wengi wanatamani wafanane na wewe kwasababu umebarikiwa na kupakwa mafuta ya kibali mbele za watu na mbele za Mungu, na siyo wafanane na waruka njia. Kama bado unaruka njia basi mtu hawezi kutamani kufanana na wewe. Mungu akubariki. 



ISIKIE SAUTI YA YESU ITAKUSAIDIA 
Ukisoma kitabu cha Waebrenia 7:25 kinasema, “ Naye kwa sababu hii anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye maana yu hai siku zote ili awaombee.” Kitabu cha Ufunuo 3:20 kinasema, “Tanzama nasimama mlangoni nabisha mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake nami nitakula pamoja naye na yeye pamoja nami.” Siku ya leo Imani imetembea, na miguu imesimama mlangoni pako. Imani inataka uifungulie mlango ili iingie kwako ili iweza kula pamoja na wewe, Imani inataka uisikie sauti yake. Je, umesikia sauti ya watu wangapi? Na hizo sauti zimekupelika wapi?

Achana na sauti ulizozisikia, sikiliza sauti ya Yesu Kristo Mnazareti ukisikia sauti ya Yesu hautapotoka tena, hautarudi nyuma tena, ugonjwa unaokusumbua utakuachilia. Tatizo la watu wengi kutosikia kusikia ya Yesu na wanasikia sauti za watu wengine, hawataki kusikia sauti ya Yesu. Ukisoma 1Yohana 11:12 inasema, “Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana anao huo uzima asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.”

 Leo wapo walio na Mwana ndani yao, kama una huyo Mwana ndani yako unauzima, umebarikiwa, umeinuliwa, Roho ya kitajiri na utulivu inaingia ndani yako. Vitu vinaharibika kwa sababu watu hawana uzima ndani yao, hata uwe mfanyakazi ni lazima uwe na uzima ndani yako. Kama Yule binti wa Israel aliye tekwa mateka akapelekwa kufanya kazi nyumbani kwa Namani, Namani alikuwa ni mtu mkuu, anaye heshimika.

Naaman alijua, alitambua kuwa Mungu ni mwenye nguvu, uweza, asiyeenda na vitu vya kutazama kwa macho. Mungu haheshimu mtu kwa sababu ana mali nyingi, Mungu anatoa heshima kwa kila mmoja uwe maskini, tajiri, mgonjwa, mlemavu Mungu anakuheshimu hivyo hivyo ulivyo.