MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCHUNGAJI: ADELLAILA LUIZA SOMO: MOYO WA SIFA

Mungu ni mwenye uweza haijalishi unapitia katika kitu gani iwe ni maumivu ya aina gani furahi maana anakupenda, unatakiwa ufurahi maana hii ni moja ya shukrani yako kwake. Filipi 4:4 “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. ” Unapofurahi unasukuma magonjwa mbali na wewe na adui yako anakimbia mbele yako. Kufurahi kwako siku zote adui yako anakuwa mdogo kuliko sisimizi, unapokuwa na huzuni adi yako ndio anafurahi bali furaha ya Mungu ni kukuona unafurahi. 
UTAMJUAJE MTU MWENYE MOYO WA SIFA AU WA SHUKRANI
 1. Anakuwa na furaha wakati wote, mtu wa aina hii siyo kwamba hana ambayo anayopita nayo hapana lakini ana moyo wa shukrani mbele za Mungu, ukifurahi mbele za Mungu hatakama unamagonjwa yanaponywa na furaha yako itakufanya uwe na Mungu kila wakati.

 2. Mtu mwenye moyo wa sifa anakuwa na shukrani, Mungu akiona una moyo wa shukrani anakupa kila kitu unacho kihitaji.

 3. Mtu mwenye moyo wa shukrani anakuwa na UPENDO wa kujipenda mwenyewe na wakupenda wengine. 1korintho 13:4-8 “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;……….. ” mtu anayependa wengine hawezi kuwaona wanalia halafu akanyamaza balia anawahurumia na kuwasaidia.

 4. Mtu mwenye moyo wa sifa wakati wote anasimulia matendo ya Mungu, 

5. Mtu mwenye moyo wa sifa hana manung’uniko wakati wote anashukuru katika kila jambo.