RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MH. MAKONDA AMTEMBELEA KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO BUGURUNI

Leo October 2 2016 Ayo TV pamoja na millardayo.com ilifika nyumba kwa kijana ambaye alipoteza macho yake mawili baada ya kuchomwa na visu na mtu aliyejulikana kuwa ni kibaka maeneo ya Buguruni.

Sid Ally alikuwa akisimulia tukio hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul makonda…’Nilikuwa natoka kazini majiri ya saa nne usiku nikawa nimesimama maeneo ya Buguruni na nunua Kuku kwa ajili ya kupeleka nyumbani ndio alipokuja mtu kwa nyuma yangu na kuomba nimsaidie‘

‘Baada ya muda yule mtu akanichoma kisu kwenye bega langu nikawa napiga kelele watu wanisaidie lakini sikupata msaada pale watu wote walikuwa wananiangali tu‘>>>Said Ally