MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA WA KANISA LA EFATHA MWENGE AKISHIRIKIANA NA WACHUNGAJI NA WATUMISHI WA MUNGU MBALIMBALI WAMEKULETEA UJUMBE UTAKAO KUBARIKI KATIKA MAISHA YAKO

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

:Jambo la msingi la kuweza kuzingatia ili uweze kupokea Roho wa Bwana.
Yohana 10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”
Roho wa Bwana ni wamuhimu sana anakusaidia wewe kumjua Mungu
Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,”
Kama umetumwa na Mungu huhitaji kumuomba yeyoto msaada bali unapaswa kumtii Yule aliyekutuma na uishi maisha matakatifu. Huhitaji kuteseka katika dunia hii kwa sababu hauna pesa au hauna mahali pa kulala.
Utajuaje kuwa watu wana Roho wa Bwana? Zaburi 126:5-6 “Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”

MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA:

Shetani akitaka kukujaribu anakuletea kitu ambacho kinafanana sana na kitu unachokipenda. Ili Mungu akutumie atakupitisha katika kila jaribu ili aone kuwa je unampenda?. Ili uweze kusonga mbele ni lazima ushinde hiyo mitihani na ukishindwa utarudia tena na tena.Aliyemuweka gerezani Yusuphu sio mke wa Potifa bali ni Mungu mwenyewe kwa kuwa alikuwa anakusudi naye, akaleta mkuu wa waoshaji na mkuu wa waokaji wakiwa wameota ndoto, Mungu alifanya hivyo kwa makusudi. Wale watu wakaja kwa Yusuphu na akawatafsiria ndoto zao, na huo ndio ukawa mlango wa Yusuphu wa kutokea, Yusuphu hakuangalia kuwa yeye ni mfungwa bali aliwasaidia. Ili Mungu akutumie ni lazima ufike eneo la ukomavu hatakama unashida kubwa kuliko za wengine unazisahau na kuwasaidia wengine. Tatizo la kila mtu ni suluhisho la tatizo la mwingine.


MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA:

Unaposhiriki mateso pamoja na Kristo, utukufu wa Mungu na Roho wake unakaa pamoja nawe. 
Mungu anataka umtolee kile ambacho unakipenda ndipo atajua kuwa unampenda, Ibrahim alipoambiwa amtoe Isaka hakuwa na maswali mengi kwa kuwa alikuwa anampenda Mungu. Ibrahim ndani ya moyo wake alikuwa tayari amemtolea Mungu Isaka kama zawadi alipotaka kumchinja ndipo malaika wakaleta kondoo. Ndipo Mungu akasema sasa nimejuakuwa unanipenda. Ili Mungu ajue kuwa unampenda ataona sadaka zako unazomtolea.
Katika mlima ambao Ibrahim alitaka kumtolea Mungu Isaka awe kama dhabihu ya kuteketezwa, ndio mlima uleule ambao Bwana Yesu alisulubiwa, Mungu alipoona Ibrahim alikuwa tayari kumtolea mwanawe wa pekee ndio Mungu akamtoa mwanawe mpendwa Yesu Kristo awe dhabihu kwa ajili ya ulimwengu.
Ili Mungu ajue kuwa unampenda toa dhabihu ambayo itamgusa. Hakuna kitakachotokea kwenye maisha yako mpaka umechukua hatua, Mungu hawezi kufanya kitu chochote kwako mpaka aone umechukua hatua ya kuanza kufanya jambo.

MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA:

Matendo 17:26-28 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone.....”
Mwanzo 39:1-5 “Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake........”
Adui zako watasababisha mteremko wa maisha yako, wa Ishmael walimtoa Yusuphu katika shimo na wakamuuza kwa Potifa ili kutimiza hatima ya Yusuphu. Maombi yangu kwako ni kwamba Mungu akupeleke mahali sahihi na kwa muda sahihi siku zote za maisha yako.

(Hapa Precious Center Kibaha).. Rumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Akili yako inaweza kutawaliwa, akili yako ikishikwa na Roho wa Mungu itakuwa salama lakini ikishikwa na ibilisi ni tatizo, ruhusu akili yako itawaliwe na Roho Mtakatifu itasababisha matokeo chanya. Kila kinachoshika akili yako kitaamua matokeo ya maisha yako. Mruhusu ROHO wa PASTOR MICHAEL OLAWORE KUTOKA UK (KATIKA KUSANYIKO KUU 2016) Mungu anatangaza mwisho tangu mwanzo, katikati ya ukame, njaa na hali ngumu isiyofuraisha MUNGU atakubariki. Yesu alikupenda hata akafa msalabani kwa ajili yako, na ni mpango wake yeye kukutoa kwenye huo ukame unaopitia. Katika hali yoyote unayopitia MUNGU hataacha kukupenda kwasababu asili yake ni Upendo na hakuna kinachoweza kumbadilisha. Mpango wa Mungu kwako ni mkubwa sana hata katika hayo maumivu unayopitia atakubariki. Amesema amekuchora kwenye viganja vya mikono yake na anakujua vizuri kiasi kwamba hata idadi ya nywele zako anaijua, na kabla hujaingia katika tumbo la mama yako alikujua. Kama hujui kama MUNGU anakupenda na kukujali ujasiri wa kuomba utapotea.
 aongoze akili yako Leo.