MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NAMSHUKURU BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KWA MAOMBEZI: 25.09.2016

Baada ya kilio cha muda mrefu sana, mama huyu aliweza kufika katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 25.10.2016 na kumshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombezi yake. Kwa kipindi kirefu alikuwa na kilio cha kupata mtoto, lakini Mungu alimjibu, na hivi ndivyo alivyosema, “Ilikuwa mwaka 2013 niliombewa na mama (Bishop Dr. Gertrude Rwakatare) kuhusu habari ya mtoto au kupata mtoto, ilipofika 2014 nikipata mtoto ambaye ni huyu hapa. Hiyo yote ni kwasababu ya madhabahu hii ya Mlima wa Moto Mikocheni ”B”. Leo nimekuja kumkabidhi mtoto huyu katika madhabahu hii ili Mungu amlinde na kumtunza. Nakushukuru sana mama, Mungu akubariki sana”. Mch. Noah Lukuma na wachungaji wengine walimuombea, “Mungu tunakushukuru kwa ajili ya mama huyu amekuja kusema ”asante” kwa kazi kubwa uliyoifanya. Mtoto huyu Bwana tunamzingira kwa damu YAKO, tunaachilia jeshi la malaika wa kumlinda, ukamlinde Bwana, wasipungukiwe kwa chochote katika jina la Yesu Kristo, tunakemea kila mwiba unaoinuka kinyume na maisha yake, tunamfunika kwa jina la Yesu Kristo. Amen