RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NI MWENDO WA KUSIFU NA KUABUDU JUMAPILI HII ARUSH


Unaposikia ya kwamba uimbaji utakuwa live basi moyo unaanza kusuuzika, unapotambua ya kwamba waandaji wa tamasha ni Habari Maalum Media basi moyo unaazaa kundunda mbiombio kuombea siku ifike mapema uwe sehemu ya wamsifuo na kumuabudu Mungu siku hiyo. Unapofahamishwa kwamba kutakuwepo na kwaya za zamani zitakuwepo pia kuhudumu ndipo unaanza kusikitika kwa nini tamasha lisifanyike hata siku mbili mfululizo...

Lakini usijali, kwa maana hata tukiimba masaa 24 hatuwezi kumaliza sifa ya Yesu, ametukuka vilivyo.

Jumapili hii tarehe 23 ndio siku inayongojewa kwa hamu kubwa na wakazi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake, kwenye ibada ya kumsifu na kumuabudu Mungu iliyopewa jina la Gospel Festival, ikishirikisha wahudumu kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo United Gospel Singers kutokea Norway, Ujerumani, Denmark, na Sweden. Waimbaji wenyeji kutoka Arusha watawakilisha vyema.

Tamasha hilo la kipekee kwa Habari Maalum Media kuandaa, litakutanisha pia viongozi wa kiroho kutoka makanisa mbalimbali Arusha, pamoja na uwakilishi wa serikali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya. Njoo wewe, njoo na mwenzako, njoo na jirani yako bila kuwaza kuhusu kiingilio, kwa maana itakuwa bure ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Na kwa wale wa nje ya Mkoa na hata nje ya nchi, basi wanaweza pia kufuatilia matangazo hayo moja kwa moja kupiti Habari Maalum FM.

Tukutane Jumapili bila kukosa...