RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA 6: ENEO LINALODAIWA KUWEPO KWA VOLCANO KAGERA, MTAALAMU ASEMA NI MOTO WA KAWAIDA


Leo October 6 2016 imeripotiwa habari ikitokea eneo la Katarabuga, kata ya Bwanjai wilaya ya Misenyi Kagera ambapo wananchi wa bonde la Katarabuga wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim Mruma amesema moto huo ni wa kawaida tu hivyo wananchi wasiwe na taharuki yoyote.

Prof. Mruma akitoa ufafanuzi juu ya uvumi huo amesema moto huo ni wa kawaida na kwamba unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi na yale majani yakiungua yanatoa kitu kama hicho. Prof. Mruma ameongeza kuwa moto wa namna hii mara nyingi unatokea kwenye makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza kuungua na ardhi inachubukachubuka kama ilivyotokea kwenye ebneo hilo.