MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

PICHA ZA MAZISHI YA MKE WA MWIMBAJI JACKSON BENTY YALIYOFANYIKA ARUSHA

Rumafrica inatoa salamu za rambirambi kwa mtumishi wa Mungu Jackson Benty kwa kufiwa na mke wake kipenzi Winnie Benty kwa ajali ya pikipiki aliyokuwa amepanda baada ya kugongwa na basi la abiria mali ya Mtei Express maeneo ya Burka, Arusha. Marehemu ameacha mjane (Jackson Benty) na watoto wawili wa kiume. Pia tunatoa pole kwa familia nzima ya Jackson Benty na wadau wa muziki muziki wa mtumishi wa Mungu Jackson. Siku ya Jumatano 12.09.2016 mwili wa marehemu Winnie Benty umepumzishwa katika nyumba yake ya kudumu makaburi ya Njiro huko jijini Arusha. 
Tunawashukuru GKkwa kuweza kutupa matukio yaliyokuwa yakiendelea Arusha kwenye msiba wa ndugu yetu. Mungu awabariki sana kwa kazi mnayofanya.

Jackson Benty akiaga mwili wa marehemu mkewe, Winnie Benty.


Sehemu ya waombolezaji.

MC Joshua Makondeko
Maombi yakiongozwa na watumishi kutoka Kanisa la Ufufuo an Uzima Tanzania.
Mama wa marehemu.
Mwili ukiagwa
Umati ukitoa heshima zao za mwisho.

Baba akibembeleza mtoto wao wa pili.
Mchungaji Bryson kutoka Ufufuo na Uzima Dar es Salaam akiongoza maombi kwenye ibada ya mazishi
Upendo Mbila kutoka CHAMUITA Arusha akimfariji Jackson Benty

Msafara kuelekea makaburini ukaanza.

Waimbaji Matilda Jojo na Tuponile Komba
Waimbaji wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania - Arusha kwa umoja wakafika baada ya kutoka studio usiku wake walipokuwa wakirekodi wimbo kwa ajili ya marehemu.

Mavumbini tutarudi
Mume wa marehemu akiweka shada la maua.

Mchungaji Frank Andrew wa Ufufuo na Uzima Arusha akiweka shada la maua kwa marehemu amnbaye alikuwa mshirika wake.


Mtoto wa kwanza wa marehemu akiweka shada la maua.
Wazazi wa marehemu
Wana Ufufuo na Uzima
Kundi la waimbaji wenza.

Safari yetu huishia hapa.

PICHA ZINGINE
xxxx