RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RAIS MAGUFULI AFANYA TENA ZIARA YA KUSHTUKIZA AIRPORT DAR ES SALAAM

 October 5 2016 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila Kabange amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake. Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.

Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa. Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.

>>>’Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua’