RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MUHIMBILI OCTOBER 3 2016


Leo October 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza  tarehe 02 Oktoba, 2016. Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.