MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

RAIS MAGUFULI ATAJWA KUWANIA TUZO YA ‘FORBES AFRICA PERSON OF THE YEAR 2016’IKIWA ni mwaka mmoja kamili tangu kuchaguliwa kwake na kuingia madarakani kuwatumikia Watanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ametajwa kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year.’

Katika tuzo hiyo, JPM anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda.

Ili kukamilika ukipagi kura, zimebaki siku 22 tu wakati hadi sasa Rais Magufuli anaongoza akiwa na asilimia 74%. Unaweza kumpigia kura Rais Magufuli kwa KUBOFYA HAPA

Mwaka huu tuzo hizo zitatolewa jijini Nairobi nchini Kenya November 17.

Wafuatao ni washindi wa tuzo hiyo miaka ya nyuma

Mohammed Dewji (Tanzania)– 2015
Aliko Dangote (Nigeria)– 2014
Akinwumi Adesina (Nigeria) – 2013
James Mwangi (Kenya) – 2012
Sanusi Lamido Sanusi (Nigeria)- 2011