RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIMBACHAWENE ATOA MIEZI 3 WAVAMIZI MAENEO YA TAASISI ZA SERIKALI KUONDOKA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene akizungumza na wanahabari.

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, ametoa miezi mitatu maagizo kwa maafisa ardhi na wakurugenzi walio chini ya mamlaka hiyo, kupima mipaka halisi ya maeneo ya taasisi hizo pamoja na kuwaondoa watakaobainika kuyavamia.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Simbachawene amesema kuwa ameamua kutoa taarifa hiyo kufuatia kukithiri kwa uvamizi wa maeneo ya taasisi za kiserikali kama kwenye shule za msingi, sekondari, vituo vya kutolea huduma za afya na masoko, unaofanywa na baadhi ya watu kwa kujenga nyumba za biashara na kuweka makazi yao ya kudumu.

Waziri huyo amewasisitizia maafisa ardhi kukamilisha zoezi hilo la upimaji kwa muda mwafaka na pia akitoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia zoezi hilo ili liweze kukamilika kwa wakati.

Alielezea kuwa anapiga marufuku biashara hizo kwenye maeneo hayo kwa kuwa zinaingilia na kuathiri utendaji na utoaji huduma wa taasisi hizo.

“Nawatahadharisha wale wote wanaojijua kuvamia maeneo hayo kuondoka mara moja kabla serikali haijawaondoa kwa nguvu,” alisema.