RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI KUFANYIKA KESHO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Hapo kesho katika kanisa kuu la CCT chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kunatarajiwa kufanyika tamasha kubwa la muziki wa injili, litakalozikutanisha kwaya kongwe na mashuhuri za kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania, Dayosisi ya mashariki na pwani kwa jimbo la Magharibi.

Tamasha hilo ambalo linafanyika siku ya Nyerere Day lipo chini ya umoja wa kwaya za Uinjilisti na Uamsho jimbo la magharibi almaarufu kama UKUU litakuwa na kiingilio cha 5000 kwa mshiriki linatarajiwa kuwa la siku nzima kuanzia asubuhi majira ya saa 3 hadi jioni sana.

Kati ya kwaya zitakazoshiriki ni pamoja na Uinjilisti Kijitonyama, Uinjilisti Safina Magomeni, Uinjilisti Sayuni Kinondoni, Uinjilisti Tumaini Msasani, Uinjilisti Tumaini Kawe, Uamsho Amkeni Kinondoni, Uamsho Kijitonyama, Uinjilisti Boko na nyingine nyingi zaidi ya 15. Ambapo mchungaji Lewis Hizza ndiye atakayekuwa mwenyeji wa kuzikaribisha kwaya hizo, ambazo hufanya tamasha mara mbili kila mwaka.