Select Menu

News

MTUME DR. PETER NYAGA

MTUME DR. PETER NYAGA

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KULIOMBEA TAIFA AMANI


Sanga Rulea 11:22 PM 0

Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Anastazia Wambura,amewaomba viongozi wa dini na waumini wa madhehebu yote nchi kushirikiana kuliombea taifa liendelee kuwa na amani na utulivu
Ametoa wito huo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki kongamano maalum la kuombea taifa amani linaloandaliwa na Kalismatic Catholic jimbo kuu la Dar es Salaam.
Akiwa kama mgeni rasmi amesema licha ya taifa kuwa na amani bado linahitaji maombezi hayo ili tunu hiyo iwe endelevu kwa maendeleo ya taifa.
“Kwanza kabisa tunachohitaji ni amani na sio serikali peke yake ina mahitaji haya, kila mwananchi anahitaji amani, kwasababu bila amani hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kikafanyika, hakuna kazi yoyote ya maendeleo wala shughuli zozote za binafsi zinazofanyika kama hakuna amani. Kwasababu tumeweza kushuhudia ambapo kikitokea tu kitu kama haya matukio ya athari watu wamekuwa wakikimbia huku na kule,kwahiyo kimsingi amani ndicho kitu cha kwanza,” alisema.
Viongozi mbalimbali wa serikali ya awamu ya tano akiwepo Rais John Magufuli, wamekuwa wakisisitiza amani na kuendelea kuwaomba viongozi wa dini nchini kuliombea taifa amani.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS