MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WANAMAOMBI WAMSHUKURU BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE SIKU YA JUMAPILI 25.09.2016

Siku ya Jumapili 25.09.2016 wanamaombi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kumzawadia Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wachungaji wa kanisa hili zawadi mbalimbali. Hii ikiwa ni kuwashukuru kwa huduma wanazozitoa kwa waumini na watu wote wanaofika kuabudu na kumtukuza Mungu katika kanisa hili. 

Pia walimshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa moyo wake wa upendo, huruma,na hekima aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.

Wanamaombi hao waliguswa sana na kitendo cha Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kanisa zima kuweza kuwatoa watungwa 78 gerezani kwa kuwalipia faini ya mil.25, hii inaonyesha ni jinsi gani Bishop pamoja na kanisa walivyo na upendo hasa kwa watu wenye uhitaji na wanaoteseka kwa kukosa watu wa kuwasaidia. 

Tuzidi kuliombea kanisa hili na watumishi wa Mungu wenye mzigo mkubwa wa kusaidia jamii katika upande wa kimwili na kiroho.

Mungu awabariki sana na tunakukaribisha katika ibada zetu kila jumapili saa 3 asubuhi na usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge