RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WASANII NYOTA AFRIKA WAAMUA KUOKOKA NA KUTANGAZA HABARI NJEMA ZA YESU


Patience Ozokwori a.k.a Mama G kampa Kristo maisha yake
Kati ya wasanii ambao suala la kuokoka kwao linaweza kusababisha mstuko wa moyo kwa mashabiki wao hasa linapokuja suala la nafasi wanazopangiwa kuigiza katika filamu kuwa za roho mbaya basi mwanamama Patience Ozokwori ama maarufu kama mama G kwenye masuala ya uigizaji anaweza kuwastusha watu, basi mashabiki wastuke tu, taarifa za kweli na kuaminika ni kwamba mwanamama huyo AMEOKOKA kwasasa.
Majid akimuombea mtu ibadani hii sio maigizo ni kweli

Mama G nyota wa Nigeria katika ugizaji ambaye asilimia 90 ya filamu alizoigiza ni za ukatili kama mama mkwe au uchawi, aliamua kumpa Kristo maisha yake mapema mwaka huu na kufanyika baraka kwa waigizaji wengine akiwemo Majid Michael kutoka Ghana ambaye alihubiriwa na mama G nakuamua kuokoka na sasa amebarikiwa na kuwa mchungaji rasmi. Licha ya mama G lakini pia kuna orodha ya waigizaji wengine watano wa Nollywood ambao kwasasa wameokoka na kuamua kujikita kwenye injili.

Aidha kwa upande wa mwanamama huyo yeye amesema licha ya kuokoka lakini hajaachana na uigizaji kwakuwa Mungu hajamwambia aachane na suala hilo, na kupinga taarifa za watu zilizosambazwa kwamba baada ya kuokoka hataki tena kuitwa mama G, mwigizaji huyo amesema si kweli na kwamba mtu yoyote akimwita kwajina hilo ataitika kama kawaida kwasababu amepewa na mashabiki wake na haoni tatizo kulitumia. Taarifa zaidi za waigizaji waliokoka akiwemo Majid Michael ambaye inadaiwa ana upako wa pekee toka siku nyingi, na hivi sasa pia amejikita katika uinjilisti basi endelea kusoma Gospel Kitaa tutakujuza kwa undani