MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WITO KWA WAKAZI DAR KUNYWA DAWA ZA MABUSHA, MATENDE


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Grace Magembe akiongea na wakazi wa Buguruni kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa Mh. Paul MakondaMkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda alipokuwa akiongea na wananchio na kuhimiza kuhusu matumizi ya dawa za kujikinga na magonjwa hayo.Mkuu wa Mkoa alikuwa mfano kwa kunywa dawa hizo mbele ya wanachi waske wa Dar es Salaam.Bibi mkazi wa Buguruni Shell naye akinywa dawa ili kuilinda afya yake dhidi ya Magonjwa hayo Hatari.

WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kunywa dawa za kujikinga na magonjwa ya mabusha, matende, usubi na minyoo ambazo zitawapa kinga dhidi ya magonjwa hayo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipokuwa akizungumza leo eneo la Buguruni Shell katika uzinduzi wa zoezi hilo la unywaji wa dawa litakalochukua siku tano ambapo amesema wagonjwa watakaopatikana na matatizo watafanyiwa upasuaji.

“Tumeandaa vituo vya afya Pugu na Mbweni Mission ambako upasuaji utakuwa unaendelea tukishirikiana na madaktari kutoka hospitali ya Muhimbili,” alisema Makonda.

Ameongeza kuwa zoezi la upasuaji litaendelea hadi mwezi wa 12 mwaka huu, ambapo hadi sasa zaidi ya wagonjwa 104 wamefanyiwa upasuaji.

“Zoezi hili tumelipa kipaumbele ili kuokoa nguvu-kazi ya taifa, tumeandaa vituo zaidi ya 281 kwa ajili ya zoezi hili hivyo wanaume kwa wanawake wajitokeze kumeza dawa hizi,” alisisitiza akiwataka pia wananchi kupuuza maneno ya mitaani kwamba dawa hizo zina madhara.

Aliwataka pia waendeleze zoezi la usafi ili kuepuka mazalia ya mbu ambapo ni vigumu kuwatambua mbu wanaoeneza ugonjwa huo.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendesha zoezi hili kuanzia mwaka 2009 ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam linatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni nne ili kuwakinga dhidi ya magonjwa hayo