RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ZINGATIA HAYA KABLA HUJAMFUNGULIA MKEO BIASHARA


katika namna moja au nyingine unaweza kujikuta katika dimbwi la uamuzi wa kutaka kumwezesha mpenzi wako kwa kutaka kumfungulia biashara kwa lengo la kumsaidiakuzalisha kipato kitakachomsaidia yeye wenyewe pamoja na familia kwa ujumla.

Kwa kawaida watu wengi wanachokifanya ni kuwapa wapenzi wao mitaji ya kuanzishabiashara bila kuzingatia uwezo na utayari wa muhusika.


Changamoto ambayo wanaume wengi wamekuwa wakikumbana nayo ni pale linapokuja suala la kumfungulia mke biashara. Ndiyo maana leo hii nimeona nizungumzie mambo ya kuzingatia pale unapojiwa na wazo hilo.

Ana uzoefu wa biashara?

Wapo wanawake ambao kwa kuwa wanawaona wenzao wanafanya biashara na wanafanikiwa na wao wanakuwa na hamu ya kuwa wafanyabiashara. Unaweza kukuta mahesabu hawajui, mbinu za biashara hawajui lakini wanalazimisha kufanya biashara.Watu kama hao ukiwafungulia biashara utakuwa unafanya kazi bure.

Lakini pia mwanaume unatakiwa kumfungulia biashara mkeo ukijua kabisa ataimudukwa kujua kuwa huenda huko nyuma alishawahi kuifanya. 

Hii kulazimisha kumfungulia duka au kumpa mtaji wa kuuza vitumbua wakati hajui aanzie wapi, faida haiwezi kuonekana na itakuwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu.


Kwa maana hiyo mke aanzishe au akubali kuanzishiwa biashara pale ambapo ataona anaimudu. Kinyume chake ni bora akafanya kazi nyingine kama kulima au akae tu nyumbani.

Yeye anataka biashara ipi?

Unaweza kuwa na wazo ya biashara fulani ambayo unaamini ukimfungulia mpenzi wakoanaweza kujiongezea kipato lakini ni vyema mtu akashirikishwa kwa kuulizwa ni biashara gani anahisi akifunguliwa ataiendesha kwa ustadi.

Nasema hivyo kwa kuwa unaweza kuwa na wazo ya kumfungulia duka au saluni lakini kumbe yeye hana uwezo wa kuendesha biashara hizo, badala yake yeye anamudu kuuza genge au biashara ya mazao. Sasa ni vyema ukamuuliza na mkakubaliana kuliko kulazimisha mtu afanye biashara ambayo haiwezi.

Utakuwa na amani?

Ukifuatilia sana wapo wanaume au wanawake ambao hawataki wake zao wafanye biashara fulani wakihisi huenda watasalitiwa. Kwa mfano ni wanaume wachache sana ambao wanaweza kuwakubalia wake zao wafanye biashara za kusafiri mikoani.

Pia ni wanaume wachache wanaoweza kuwafungulia wake zao biashara ya baa, kwa nini? Kwa sababu wanahisi hawatakuwa na amani mioyoni mwao.


Ndiyo maana nikasema biashara ambayo utamfungulia mpenzi wako isije ikaleta migogoro na kuwafanya mkawa ni watu wa kutibuana kila wakati. Itakuwa ni jambo la ajabu kama utakubali mpenzi wako afanye biashara ya kuuza kwa mkopo nguo za kikehalafu ukawa hutaki awe ni mtu wa kuzurura kwenye nyumba za watu. Au unamruhusu afanye biashara ya baa halafu unataka awahi kurudi nyumbani, hapo hiyo biashara itafanyikaje?

Atamudu biashara na familia?

Sote tunajua kuwa mke ni mtu muhimu sana katika malezi ya familia hivyo unapomuanzishia biashara ujiulize ataimudu pamoja na kulea familia vizuri? Isije ikawa unamuanzishia biashara halafu ukitaka mtafute mtoto anakuambia msubiri kwanza, au kwa kuwa anafanya biashara basi haijali familia, yeye muda wote anakimbizana na pesa, hiyo haitakuwa sawa!

Kwa nini biashara?

Siyo kila mtu anaweza kufanya biashara, wengine ukiwafungulia biashara utakuwa unacheza kamari. Kwa maana hiyo ifike mahali ujiulize ni kwa nini umfungulie biashara mkeo? Jibu la swali hilo litakupa muongozo.