MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

06.11.2016: WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ANISET BUTATI NA KASAKI SELEMANI WALIVYOMTUKUZA MUNGU SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 06.11.2016 mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Aniset Butati pamoja na Kasaki Selemani waliweza kumsifu Mungu kwa nyimbo zao zenye upako wa ajabu katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" chini ya Bishop Dr. Gertude Rwakatare. 


Watu wengi walivutiwa na kubarikiwa na uimbaji wao kutokana na ujumbe uliomo katika nyimbo zao. Kila wanaposhiriki ibada ya Mlima wa MOto MIkocheni "B" wamefanyika baraka kwa kila mtu. 


Mungu azidi kuwabariki katika huduma yao ya kumtumikia Mungu.Nyimbo zao zimeinua imani za watu na kuwa karibu na Mungu, kila wanapoimba kunakuwa na wingu la uwepo wa Mungu.

Tunakukaribisha katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B". Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa utaona mabasi ya Mlima wa Moto MIkocheni "B" au utasikia watu wakisema "kwa mama " ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.