RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

13.11.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AZIDI KUWABATIZA WATU KWA WINGI, NA SIKU YA JUMAPILI WENGI WALIJITOKEZA KUBATIZWA KWA MAJI MENGI

Jumapili 13.11.2016 ilikuwa ni Ibada ya kupakwa mafuta ya upako yalioombewa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa kanisa hilo akiwemo Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Noah Lukumay, Mch. Francis Machichi, Mch. Mama Mgetha, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Stanley Nnko n na watumishi mbalimbali walioshiriki katika kuyaombea mafuta haya wakiwa kanisani au majumbani mwao, na pia kila mtu aliyefanya maombi binafsi kabla ya kupakwa mafuta hayo.
Kabla ya kupakwa mafuta ya upako Mch. Elizabeth Lucas aliweza kutoa nafasi kwa watu wanaohitaji kuokoka ili wampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Tunamshukuru sana Mungu watu wengi walijitokeza na kuamua kuokoka. Mch. Elizabeth Lucas aliongoza sala ya toba na baadae Mch. Francis Machichi, Mch. Stanley Nnko, Mch. Mama Mgetha, na wainjilisti wa kanisa hilo waliweza kuwaombea.
Baada ya kumaliza zoezi hili la maombezi, watu wote waliweza kupakwa mafuta ya upako na kuombewa na baadae wale waliokoka walipelekwa kubatizwa UBATIZO wa maji mengi baharini. Wakati wakibatizwa watu wengi waliguswa na nguvu za Mungu, wengine walitokwa na nguvu za giza na wakajazwa Roho Mtakatifu. Siku ya Jumanne waliendelea na masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Sasa ni zamu yako ndugu yangu kuja kwa Yesu. Maisha yetu ya kuishi hapa duniani hayana formula, kwani hatujui ni jambo gani litatukumba hapo baadae. Ni vyema sasa ukachukua uamuzi wa kuokoka na kumtumikia huyu Bwana wetu Yesu Kristo.
Yawezekana unapitia magumu fulani na huoni mtu wa kukushika mkono, lakini nataka ni kwambie ukiwa na Yesu utashangaa unapata mpenyo wa kimaisha.Utashangaa Mungu anakuinulia watu wa kukusaidia katika majaribu yako.
Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho, nje kidogo utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" au fika Mwenge mataa barabara ya Coca Cola utasikia watu wakisema kwa mama. Mungu akubariki sana na usisahau kutembelea blogu yetu  www.mountainoffiretanzania.blogspot.com au kusikiliza Praise Power 9.3FM au kuangalia Channel Ten kipindi cha SAA YA FARAJA KILA ALHAMISI SAA 3:30 USIKU












































































 Mwinjilisti Ngugi






 Mwinjilisti Asenga



 Asenga akiongea na mtumishi aliyeamua kukoka akitokea dini ambayo sio ya Kikristo, na sasa ameamua kumpokea Yesu Kristo. Kilichomgusa sana na kuamua kukokoa anasema ni yale mafundisho ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare