MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

13.11.2016: CREW YA PRAISE POWER RADIO 99.3 FM WATEMBEA MTAA KWA MTAA KUKUHIMIZA WEWE KUHUDHUURIA IBADA YA KIHISTORIA YA KUPAKWA MAFUTA SIKU YA JUMAPILI HII KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Siku ya leo watangazaji wa Praise Power Radio (PPR) 99.3 FM walikuwa mtaani wakihimiza watu kufika katika Ibada ya KUPAKWA MAFUTA itakayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lililopo jijini Dar es Salaam kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Ibada hii yenye upako wa ajabu itaanza rasmi saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Haya ni masaa machache yatakayobadilisha historia ya maisha yako ukiamini na kuzidi kukaa katika miguu ya Bwana.


Yawezekana wewe unapitia magumu na yamesababisha hali yako kuyumba, pengine shida yako ni kupata mke/mume, kazi nzuri, kupandishwa cheo, kuongezewa mshahara, kufanya vizuri masomo yako, kupata kiwanja, kujenga nyumba yako, kupata mke/mue mwema na sio ili mradi mume/mke, kupata mchumba, kuinuka kiimani, kusoma Neno la Mungu, kupata kibali, kupona magonjwa yanayokusumbua kwa muda mrefu, kutolewa mapepo na majini yanayokusumbua katika maisha yako, kutoota ndoto mbaya na chafu, kutoangalia picha chafu mitandaoni, kujinasua katika mtego wa kutekwa nafsi yako, kukumbukwa na Bwana, kuvunja nira za shetani, kuheshimika, kupendwa na watu, kuwa na hamu ya kutamani kujua sana Neno la Mungu na kuhudhuria ibada na mambo mengine kama hayo. 

Mtangazaji wa PPR Bony Magupa

Basi Jumapili hii baada ya kuombewa na kutubu dhambi zako, utapakwa mafuta yalioyoombewa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa wiki nzima na ukiamini kuwa kupitia mafuta haya unaenda kufunguliwa, basi hiyo imani yako itakuondoa katika mateso unayopitia. Kwahiyo hii ni ibada ya kutokosa kabisa mtu wa Mungu.


Mungu wetu ni Mungu wa huruma na upendo, anatamani sana kukuona wewe unafurahia wokovu wako na maisha yako kwa ujumla. Inawezekana wewe ulitamani kubatizwa, basi kesho utapata muda wa kubatizwa kwa maji mengi na utapokea Roho Mtakatifu.


Ninachotaka kusema ni kwamba ibada hii si ya kukosa kwani kufika kwako kutasababisha mambo mengi sana kubadilika katika maisha yako.


Kuna watu wengine wana maisha mazuri sana, lakini hawana amani na mali zao, wanaishi kama watu masikini, na hii ni kwasababu shetani ameingia katika kisima cha furaha yao, kisima cha maisha yao, kiima cha maendeleo yao na kutibua yale maji safi na kuwaachia maji machafu yanayosababisha amani na furaha kutoweka katika maisha yao. Basi Jumapili hii Bwana anakwenda kukusaidia katika tatizo lako hilo. Wewe njoo ukiwa umeachia moyo wako kwa Yesu na kusema Yesu nisaidie katika hili ninalopitia. 


Mungu akubariki sana na kesho tuonane Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi. Kuhusu usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabsi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utayaona magri ya Mlima wa Moto Mikocheni "B", na baada ya ibada utarudishwa pale walipokuchukua. Ubarikiwe na Bwana.

Mtangazaji wa PPR Hosein Gabriel (kushoto)