MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

16.11.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOA MISAADA MBALIMBALI KWA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA – MOI MUHIMBILI SIKU YA JUMATANOBishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumatano 16.11.2016 aliweza kuwatembelea, kuwafariji, kuwaombea na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na wazee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakipakia zawadi kwaajili ya watoto wenye vichwa vikubwa.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alipofika katika hospitalini hapo aliumia sana kuona watoto wadogo wakiteseka na ugonjwa huu wa kujaa maji katika vichwa vyao na kusababisha vichwa kuwa vikubwa sana. Pia aliwatia moyo wazazi wa watoto hawa ya kwamba wasikate tamaa kwani Mungu yupo atakaye watetea katika kpindi hiki kigumu wanachopitia cha kuwauguza watoto wao. 

Pia alisikitika kusikia kuwa kuna baadhi ya wazazi wa watoto hao wametengwa na familia zao na wengine waume zao wamewakimbia eti kwasababu wamezaa watoto wenye vichwa vikubwa, na hii imesababisha wazazi hawa kupatwa na usongo wa mawazo wa jinsi gani wanaweza kuwalea hawa watoto wenye vichwa vikubwa. Akina mama hawa walionekana wakilia kwa machozi kutokana na changamoto wanazopitia katika kuwauguza watoto wao huku wengine wakiwa wamekosa msaada kutoka katika familia zao au waume zaoBishop Dr. Gertrude Rwakatare alisikitika sana kuona wazazi walio wengi hapo hospitalini wana shida ya mahitaji mbalimbali, na hii ni kutokana na kukaa muda mrefu hospitalini wakiuguza watoto wao huku wakishindwa kupata muda wa kwenda kufanya kazi ili wajipatie kipato.

Kwahiyo kutokana na hivyo aliweza kutoa pesa na misaada mbalimbali ili iwasaidie katika kipindi hiki kigumu kwao na aliwaomba watu wajitokeze kuwasaidia hawa watoto kwani wanahitaji mahitaji mbalimbali katika afya zao.


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akipeleka misaada wodini kwa watoto wenye vichwa vikubwa.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwatia moyo wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa
 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akimuombea mtoto mwenye kichwa kikubwa

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akimuombea mtoto mwenye kichwa kikubwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akimfariji mtoto menye ugonjwa wa kichwa kikubwa