MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

30.10.2016: BISHO DR. GERTRUDE RWAKATARE AWAOMBEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WANAOTEGEMEA KUFANYA MITIHANI YAO YA MWISHO


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 30.10.2016 katika tamasha la maombi lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” aliweza kuwaombea wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne. Baadhi ya wanafunzi walikuja na vitendea kazi kama vile pen, daftari n.k.
Pia baadhi ya wazazi ambao hawakuja na watoto wao katika ibada hii waliweza kuombewa kwa niaba yao. Kama mkristo unaombwa kushiriki kuwaombea wanafunzi hawa ili wakaweze kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.
Pia tungependa kukukaribisha katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni “B” kila Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki kuanzia saa 9 mchana hadi usiku.

Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi Makumbusho na Mwenge wote mnakaribishwa