RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

30.10.2016: KWAYA YA JOYBRINGERS NA HAPPY KWAYA ZAWABARIKI WAUMINI NA WAGENI WALIOFIKA KATIKA TAMASHA LA MAOMBI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B” JUMAPILI HII

Kwaya ya Joybringes na Happy kwaya siku ya Jumapili 30.10.2016 zilifanyika Baraka kwa waliobahatika kuhudhuria ibada ya Jumapili. Kupitia uimbaji wao watu waliweza kubarikiwa kwa nyimbo zao na jinsi wanavyojituma katika suala zima la kumsifu Mungu. 

Watu wengi walibarikiwa na uimbaji wao mpaka ikafikia kipindi wakashindwa kujizuia kukaa kwenye viti vyao ikabidi wainuke na kwenda kuwapongeza kwa zawadi mbalimbali, nah ii inatokana na kuguswa na ujumbe waliokuwa wanautoa kwa njia ya uimbaji.
 
Tunakukaribisha wewe ambaye umewahi kufika au hujawahi ila unasikia habari za Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa njia mbalimbali. 

Tunaamini kupitia waimbaji hawa Mungu ataongea na wewe kwa njia ya nyimbo na utaondoka ukiwa fikra tofauti na ulivyoingia. Tunakuomba ikiwezekana njoo na rafiki au ndugu yako ili na yeye abarikiwe kama utakavyobarikiwa. 
 
Ibada zetu zinaanza saa3 asubuhi hadi saa 8 mchana siku ya Jumapili na katikati ya wiki tunaanzia saa 9 mchana hadi usiku. Mungu akubariki