RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

30.10.2016 : MCH. FRANCIS MACHICHI AFUNDISHA JUU NGUVU YA MAOMBI YA KANISA KATIKA TAMASHA LA MAOMBI LILILOFANYIKA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”


Mch. Francis Machichi wan kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 30.10.2016 katika ibada ya Tamasha la Maombi alikuwa na haya ya kusema kwaajili yetu, alisema, “Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Askofu wetu kupanga siku ya tamasha ya maombi, kanisa bila maombi hakuna safari ya muda mrefu. Maombi ni akiba kwaajili ya kazi ya Mungu, kwaajili ya maisha yetu ya kiroho. 
Siku ya leo ni siku ya tamasha ya maombi wewe uliyekuja kanisani Mlima wa Moto Mikocheni ”B” nataka niongee kidogo tu kuhusu Nguvu ya Maombi ya kanisa. Tusome Matendo ya Mitume 12:5 “Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.” 

Biblia inasema Petro aliwekwa gerezani na Herode, Herode alikuwa na tabia ya kuwanyanyasa watumishi wa Mungu, kulitesa kanisa, kuwaua watumishi wa Mungu. Biblia inasema, huyu Herode alimuua Yakobo, Yohana, akamuweka gerezani. Lakini kanisa liliposikia Petro ameenda gerezani, kanisa likakaa na kuomba. 
Maombi ambayo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anatangaza ya kanisa kuanza kuyafanya kwa mwezi mzima hayakuanza leo yalianza toka wakati ule Petro alipoingia gerezani. Kwahiyo maombi yakitangazwa kanisani siyo ya mtu binafsi ni maombi ambayo yapo kwenye Biblia. Biblia inasema, “Kanisa litasimama kufunga na kuomba.”

 Inawezekana wewe hujaenda gerezani Segerea kama Petro lakini katika maisha yako ya kila siku unahitaji maombi ya kanisa kwasababu kuna mambo yako yamefungwa, maisha yako, miradi yako, maendeleo yako yamefungwa, kwahiyo unahitaji maombi ya kanisa. Na ndio maana ratiba kuwa mwezi wa 11 utakuwa ni mwezi wa maombi ambayo yatakuwa ya kanisa zima.


Unaweza kuwa wewe ni muombaji mzuri, unaomba peke yako, wakati mwingine mambo yako yanakuwa mazito unashindwa kuomba, hapo unahitaji maombi ya kanisa ndio maana Waebrania 10:25 inasema, ”Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine bali tuonyane, na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.” Wakati mtu ameshindwa anahitaji mwingine wa kumtia nguvu. Hatukusanyiki kwasasabu ya desturi bali kwa kuombeana maana wakati mtu ameinama moyo anahitaji mwingine wa kumtia nguvu, mtu ameshindwa anahitaji mwingine wa kumbeba, mtu analia hawezi kuomba. Kuna wakati wa mapito mazito huwezi kuomba unahitaji kuombewa.
Wiki hii niliumwa nyumbani nikajisikia vibaya, sikuweza kabisa lakini namshukuru Mungu kwa sababu kuna timu ya watu wa maombi humu ndani wakanisaidia sasa leo nimesimama nikiwa na nguvu. Bwana anatenda kwani maombi ya kanisa yanauwezo wa kukugusa mahali ulipo. Biblia inasema, “Petro akawekwa kizuwizini kanisa lilikuwa likiomba”. 


Neno la Mungu linasema hata Herode alipokuwa anataka kumtoa Petro usiku kucha Petro alikuwa amelala katikati ya askari wawili, Petro alipokuwa kizuwizia alikuwa amelala maana alikuwa amefungwa, lakini kanisa lilikuwa linaomba. Yawezekana una matatizo ambayo huwezi kuomba, unaomba maombi hafifu, unalala bila kuomba, leo ni tamasha la maombi lazima kanisa lisimame, katika shida uliyonayotuombe kwa pamoja kama ilivyofanyika kwa Petro.


Petro alikuwa analala amefungwa minyororo miwili kwaajili ya ulinzi. Petro hakuwa kwenye mazingira ya kuomba wala makazi ya kuomba, ndio maana kanisa lilichuku a jukumu la kumuombea. Ndio maana leo kanisa linatangaza maombi kwa ajili yako kwasababu wewe umebanwa unahitaji kuombewa tu. Inawezekana upo kwenye kipango cha madeni hauwezi kuomba, maombi hayapandi, unaumwa una maumivu, maombi hayapandi, unalia una matatizo maombi haya pandi, lakini Biblia inasema, ”Kwa maombi ya kanisa lazima utatoka mahali ulipo” Biblia inasema, “Petro alikuwa gerezani, alikuwa amekata tamaa, walinzi walikuwa wanamlinda na amefungwa minyororo lakini baada ya kuombewa akapata mpenyo .”


Yawezeka mtu wa Mungu uliyeingia kanisani hapa umefungwa na mila za kwenu, roho za kwenu, madeni na Mganga wa kienyeji amekubana na unashindwa hata kufanya maombi binafsi”. Habari njema ni kwamba maombi ya kanisa ambayo yametangazwa leo na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ya mwezi mzima wa 11, lazima Bwana anakwenda kukutoa mahali ulipo kwa jina la Yesu. Biblia inasema, “Mara malaika wa Bwana akasimama karibu na Petro, nuru ikamwita kule chumbani, ikampiga Petro ubavuni, ikamuamsha ikisema ondoka upesi minyororo yake ikamwanguka.” Petro alikuwa amefungwa lakini kwa sababu ya maombi ya kanisa Petro akatokewa na malaika akamwambia amka ondoka alipotaka kuondoka akaona minyororo yake ikamuachia. 


Leo naomba minyororo iliyokushikilia kwenye matatizo, magonjwa inaenda kukuachia maana malaika wa Bwana anaenda kukuamsha, ondoka kwenye kitanzi ya madeni, kwenye kitanda cha magonjwa umelia sasa imatosha, namuona malaika akiingia chumbani kwako, ofisini kwako ili kukuinua mahali ulipo shindwa. Malaika lazima aingilie kati kwenye shida yako tamasha la maombi la leo lazima malaika waonekane kwako Petro hakuomba, lakini kanisa liliomba, wewe yawezekana hautaomba lakini kwa maombi ya kanisa shida yako lazima ipate kutatuliwa nawaona watu shida zao zikitatuliwa, nawaona watu minyororo ikiwaachia, wewe umefungwa na minyororo ya madeni, kuonewa, kutoa kuzaa, kutokuolewa, kwenye maombi ya kanisa namuona Bwana akiingilia, namuona malaika akiingilia kati katika jina la Yesu. 
Malaika akamwambia jifunge kavae viatu vyako Petro aliuwa kalala ghafla akaambiwa na malaika jifunge kavae viatu, kwa hiyo maombi yana uwezo wa kuingilia kati katika shida uliyo nayo. Namuona mtu akiinuka. Petro alimuona malaika kwa sababu ya maombi ya kanisa alimuona malaika akimwambia, “Ondoka” hakuamini, minyororo ikamuachia. Nawaona wale wanaokulinda kule kijijini kwenu, wanaonuwiza kwa ajili yako, wanasema ameenda kule mjini sawa, lakini mafanikio kule mjini hatapata, na muda wake kule mjini ni miaka minne, atarudi hapa kijijini kulima mashamba, hao wanaokulinda huko kijijini leo ninawaachia usingizi mzito, malaika wa bwana akunyanyue akupitishe katikati yao kwa jina la Yesu.


“Yawezekana umesimama mahali fulani ambapo unaona hakuna njia, mpenyo, matumaini, sauti, kelele lakini namuona malaika akikutoa mahali pale kukupeleka katika shina la Yesu kristo. Petro aliona kama anaota ndoto akiwa amefungwa lakini Mungu alimuona na hii itakuwa na kwako kwa jina la Yesu. 

Bwana anakwenda kukugusa na waliokucheka wataona ukiinuka hiyo ni nguvu ya maombi ya kanisa, Petro hakufunga siku hiyo, hakuomba, hakufanya lolote alichokifanya aliji ” connect” na kanisa na kilichomsaidia ni maombi ya kanisa ambayo yakamgusa. Sasa s sema, “Hata mimi nitaguswa na maombi ya kanisa”. Nguvu ya maombi ya kanisa yanaweza kubadilisha maisha yako. Biblia inasema, “Petro akakaa, haelewi, akaona kama ndoto lakini tayari alikuwa ameshafunguliwa, hata Petro alipopata fahamu.” 
Hata na wewe yawezekana fahamu yako imepotea huoni msaada lakini leo Mungu anakwenda kukupa ufahamu wa kujifungua katika mateso yako. Pengine Bishop Dr. Gerude Rwakatare anakuambia, “Shika kichwa chako” lakini wewe unaangalia tu bila kushika kichwa chako kwa imani ili upokee muujiza wako. Kunauwezekano wa fahamu zako kufungwa na shetani, Ninawaona watu mahali hapa fahamu zao zikifunguka naona miradi mikubwa kwa sababu Bwana anaenda kufungua fahamu zao.


Petro baada ya kufunguliwa na kuwekwa huru akasema, “Sasa nimejua ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa Taifa la wayahudi”, Petro alivyoenda huku alipopita kwenye hiyo nyumba aliwakuta watu huku ndani wengi wakiomba. Walinzi wakasikia mlango unabisha wakaogopa wenyewe kufungua maana waliangalia alipofungwa Petro hawezi kutolewa klwa maana wanaijua tabia ya Herode ya kuchinja, kuua lakini walipo isikia sauti yake mlangoni wakaogopo. Ninaona watu walio kufunga usiendelee wakiogopa wakati watakapokuona unaendesha gari yako, naona mbingu zikifunguka kwa ajili yako wewe uliyeshiriki ibada ya Tamasha la Maombi siku ya leo. 

Mlinzi aliposikia sauti ya Petro alishindwa hakufungua kwakuwa aliogopa akapeleka kwanza taarifa akasema, Nimesikia sauti lakini hii sauti ni ya yule mtu tunaye muombea. Hakufungua mlango kwa ajili ya furaha bali alipiga mbio akaingia ndani akawambia kwamba, “Petro amesimama mbele ya lango” wakamwambia, “Wewe unawazimu!” Naona watu wanatukanana kwaajili yako maana Bwana anaenda kukuinua watu watasema wewe unawazimu, hilo gari unaloendesha sio la kwako, huyu mke wake amemuoa siyo wa kwake, hiyo kazi anayofanya hakustahili, huyu hawezi kuwa Mbunge. Naona Bwana akikuinua na watu wakigombana kwa ajili yako. Wakanena wewe unakichaa, ni malaika wake, siyo Petro. Wakati unaendesha gari watu watasema siyo yeye ni mzimu wake umetokea tunavyo mjua hawezi kuendesha gari, tunavyo mjua hawezi kuolewa, hawezi kupata kazi.


Baada ya Petro kutoka kwenye kifungo baadhi ya watu wakasema, ”Siyo Petro au ni mzimu wa Petro umetokea?” Lakini nataka nitangaze kwenye tamasha hili la maombi linalofanyika Mlima wa Moto Mikocheni siku ya leo, watu wanaenda kupata raha kwa sababu Bwana anaenda kuwatendea mema, Bwana anaenda kuonekana kwao, watu wanakwenda kushangazwa, watajiuliza, “Siyo yeye yule?” Biblia inasema wakamuona Petro wakastaajabu wakasema, “Siyo Petro?” Petro akasema, “Mnanichelewesha ni mimi Petro na sio mzimu”. Naona watu wakistaajabu wakati Bwana akikupandisha viwango. Bwana anaenda kukuponya na magonjwa yako yote. Nasema, “Bwana akikuinua waliokuonea watakukaribisha sasa, waliokuonea watakupa kiti ukae, waliosema hutainuka watakuona upo mbele, waliosema hawezi watakuona unaweza.” 


Biblia inasema, “Kwa sababu yule Herode hakutambua maombi ya kanisa juu ya Petro akafa, kwahiyo maombi yana nguvu ya ajabu sana”. Nawaona wale waliokufunga magerezani, wale waliokusababisha usiinuke, wale waliokufanya usipate kazi wanaachilia kwa jina la Yesu Kristo. Kuna nguvu ya mombi ya kanisa, kuna nguvu ndani ya maombi ya kufunga, ukisikia mtumisha wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anatangaza maombi ya kanisa naomba uyazingatie na utii. Petro hakufunga pamoja na kwamba alifungwa gerezani, kanisa lilifunga kwaajili yake na kuomba na hatimaye alipata kuwa huru. na wewe ukifunga kwaajili ya wengine nao watafunguliwa katika familia yao, maisha yao kwa ujumla kwa kupitia nguvu ya maombi ya kanisa.

Hebu angalia miguu yako inayokuwezesha kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Unajua ili uweze kutoka Musoma kuja Dar es salaam lazima utumie hiyo miguu yako, sasa kuna wengine miguu yao imefungwa minyororo, maisha yao yamefungwa na shetani, lakini kwa maombi ya leo unaenda kumwambia Bwana kwamba, Mahali ambapo sikufika kwa sababu ya minyororo ya wanadamu, nahitaji nikafike sasa, hatima yangu ambayo imezuiliwa na wanadamu kwa sababu wameiweka gerezani, kwa mombi ya leo Bwana naomba nikaifikie hatima yangu. 
Sasa naomba tuombe, ”Sema ee miguu yangu, wewe umekombolewa na damu ya Yesu, wewe ni wathamani, na leo naongea na wewe kama kuna minyororo, kama kuna uchawi iliyokuzuia ili usiende kwenye hatima yako. Leo nakata minyororo iliyokuzuia ili usiendelee, ili usifike mbali, ili usifanikiwe, leo ni mwisho kila minyororo iliyoshika maisha yako yasiendelee ninaikata kwa jina la Yesu. Sema, Amen.”Baada ya maombezi Bishop Dr. Gertrude aliweza kutamka maneno ya baraka, alisema “Peleka mikono yako mbele kama unapokea kitu, iunganishe vitu visidondoke, mikono yako imekuwa ikipoteza, kila unachoshika inaharibu, ulianza mradi ukafa, ulianza kujenga likabaki pagale, ulipewa mkopo wa biashara mkopo wote ukaliwa ukaisha, biashara ikafa mikono yako ni ya kupoteza ulipewa hela ukatapeliwa leo kwa jina la Yesu unakwenda kufunguliwa na kupokea Muujiza wako.



MAOMBI
Mch. Francis Machichi baada ya kufundisha somo la NGUVU YA MAOMBI YA KANISA aliweza kufanya maombi, na hivi ndivyo alivyoomba, “Sema milango itafunguka, kwenye tamasha la leo Maombi, lazima milango ifunguke”, Tunaenda kufanya maombi ya milango iliyofungwa katika maisha yako kufunguliwa. ili uingie mahali panapo stahili, inua mikono yako sema maneno haya, ”Ee Bwana Yesu kwenye tamasha hili la Maombi kila mlango uliofungwa mbele yangu, kila gereza lililonifunga, kila kaburi lililochibwa ilikunizika ninavifungua na kuvifunika kwa damu la Yesu. Waliotamka mabaya kinyume na maisha yangu wataniona nikitokelezea kwa jina la Yesu. Wewe shetani leo nimekungundua umenifungia milango, sasa nachukua Baraka hii naenda kuifungua milango yote leo nafungua kwa jina la Yesu. Sasa ninaomba kila mmoja aweza kuomba akimwambia Mungu afungue kile unachoona kimefungwa na shetani katika maisha yako, anza kuomba sasa....