RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

30.10.2016: MCH. STANLEY NNKO AONGOZA MAOMBI YA KUWAOMBEA WATOTO WANAOPITIA CHANGAMOTO MBALIMBALI SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na Mch. Stanley Nnko siku ya Jumapili 30.10. 2016 katika ibada ya Tamasha la Maombi lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” waliweza kuwaombea watoto ambao wanaishi maisha yasiyompendeza Mungu kutokana na sababu mbalimbali, Mch. Stanley Nnko alisema, 


“Tutaomba kwa ajili ya watoto wetu wengine mmewapeleka watoto kwa bibi zao wanalelewa huko vijijini na haujui wanaishi mazingira gani. Ni vizuri tukawaombea watoto wetu popote walipo. Kama una watoto wako ni vyema ukawaombea maana wanapitia changamoto nyingi, ombea watoto wako wanao soma, wasio na heshima, waliofukuzwa, yatima, walioamua kuhama kutokana na migogoro ya wazazi, waliologwa n.k. 

Watoto wengine wananyanyaswa, waonewa, wanateseka, wanaishi kwenye nyumba za ajabu mitaani, hawana makazi wanalala nje. Kuna watu wengine hawaoni uchungu wa watoto wao, wamekamatwa na gereza la ulevi, makundi mabaya, kuvuta bangi, ngono, utukanaji kwasababu wazazi wao wameharibu “future” yao au mtazamo wa maisha yao ya baadae. 


Lakini leo tunawaleta watoto wetu kwa Yesu, sasa naomba tuombe, sema, ”Ee Bwana Yesu tunakusii watoto hawa wabadilishe, waokoe wakawe wema na kurudi majumbani mwao au kuwa na tabia njema. Bwana ponya kanisa lako, watoto wako, watoto wetu, wafundishe Bwana namna ya kuenenda kwa jina la Yesu Kristo. Asante Bwana maana unakwenda kutenda.” Endelea kuomba..