RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BI CLINTON AMESEMA FBI NDIO CHANZO CHA YEYE KUSHINDWA UCHAGUZI WA NOVEMBA 8, 2016


Aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tikiti ya Chama cha Democratic Hillary Clinton, amesema kwamba kushindwa kwake ghafla katika uchaguzi uliyopita, kulichangiwa pakubwa na hatua ya mkurugenzi wa shirika la kijesusi la Marekani FBI, James Comey kutangaza uchunguzi mpya wa sakata ya barua pepe dhidi yake muda mfupi kabla ya uchaguzi.

Bi Clinton amewaambia wafadhili wa chama chake kwamba hatua ya Comey ilisambaratisha kampeini yake, licha ya uchunguzi huo kutompata na hatia.


Mkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI James Comey