TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOA MISAADA KWA WAGONJWA WA KANSA (CANCER) KATIKA HOSPITALI YA OCEAN ROAD

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Ijumaa 18.11.2016 aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kansa (cancer) katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Pia aliweza kufanya maombi na kuwatia moyo wagonjwa ambao walionekana wakilia kila wakati kutokana na mateso wanayopitia. Baadhi yao wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu kwa muda mrefu sana huku wakiteseka. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akimtia moyo mgonjwa katika hospital ya Ocean Road

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwashukuru waaguzi wa hospitali hiyo kwa huduma yao na upendo wao wanaoonyesha kwa wagonjwa hawa ambao ukiwaona utawaonea huruma jinsi wanavyoteseka. 

Wagonjwa walifarijika sana pale tu mtumishi wa Mungu Dr. Gertrude Rwakatare alipowaombea na kugawa zawadi kwaajili ya mahitaji yao mbalimbali. 

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiongea kwa uchungu mkubwa hapo hospitalini alisema, "Hawa ndugu zetu wanateseka sana, wanahitaji kusaidiwa kimwili na kiroho ili waweze kupona na waishi maisha ambayo sisi tuliowazima tunayaishi. 
Hawatamani kabisa kuishi maisha ya mateso na kuwa tegemezi kwa wengine. Ni jukumu letu sisi tuliowazima kuwaombea hawa ndugu zetu, kuwatia moyo, kuwafariji na kuwasaidia kwa kile kidogo tunachobarikiwa na Mungu.Pia tuwatembelee hawa wagonjwa kwani wengine wamekuwa wapweke kabisa."

Baada ya kumaliza zoezi la kuwaombea na kugawa misaada, wauguzi waliweza kumshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kitendo alichokifaya cha kutoa misaada hapo hospitalini, pia wagonjwa walimshukuru sana kwa kupata misaada hiyo.