RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BUSUNGU ANUSURIKA KIFO AJALINI DAKAWA




Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Malimi Busungu amenusurika kifo katika ajali ya gari jana jioni katika eneo la Dakawa akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma.

Menaja wa mshambuliaji huyo akithibitisha ajali hiyo alisema; “Kweli Busungu kapata ajali, na gari imeharibika vibaya sana. Ila Busungu mwenyewe amenusurika na yuko salama.”

Baadaye mshambuliaji huyo naye alithibitisha kutokea ajali hiyo lakini akamshukuru Mungu kwa kumnusuru na kutoka salama katika ajali hiyo.