RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ETIHAD YATUNUKIWA TUZO YA WASAFIRASHAJI BORA AFRIKA


Shirika la Ndege la Etihad limeshinda tuzo ya ubora ya usafirishaji kwa daraja la kwanza na wasafirishaji bora wa mizigo kwa ndege katika Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika kwa ujumla kupitia tuzo za ubora za AirlineRatings.com 2017. Shirika hilo lenye makao makuu yake makuu Abudhabi, pia limetajwa kuwapo kwenye kumi bora duniani kutokana na ubora wa hali ya juu wa huduma zake.

Mhariri Mtendaji wa AirlineRatings.com, Geoffrey Thomas alisema,” Shirika la Ndege la Etihad limeibuka mshindi wa tuzo hizo na kuwa mshindi wa kwanza kwa utoaji huduma daraja la kwanza na usafirishaji wa mizigo Mashariki ya kati na Afrika kwa ujumla pamoja na kuingia kwenye kumi bora za AirlineRatings.com ulimwenguni kote, kutokana na ubora wa huduma zake.”

Alisema, “Hili ni jambo la kujivunia kwa kushinda tuzo ya Airlineratings.com na Shirika la ndege la Etihad ndilo limeingia kwenye kumbukumbu ya kushinda maeneo matatu tofauti kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo”

“Shirika hili la ndege limekuwa la kipekee pia kwa kufanikiwa kupata hadhi ya juu kwa bidhaa na usalama kupitia Airlineratings.com,” alisema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “ Ushindi wa tuzo hii ya ubora kwa daraja la kwanza na wasafirishaji mahiri wa mizigo Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika kwa ujumla kwa miaka mitatu mfululizo ni jambo kubwa la heshima kuendelea kujizatiti na kuongoza kwenye ubora wa bidhaa, huduma zinazotolewa za kiwango cha juu ulimwenguni.”

“Zawadi hii inatuhamasisha kuendelea kufanya vyema katika sekta ya anga na kuongeza ubunifu na utendaji kazi pamoja na kuimarisha usalama, jambo ambalo linatufanya kuendelea kuwa wa kwanza kwa ubora,” alisema.

Tuzo ya The 2017 AirlineRatings.com imekuja ikiwa ni baada ya wiki chac he zilizopita baada ya kupokea nyingine kutoka kwa Skytrax Certified 5-Star Airline Rating. Tuzo hizo za Skytrax zilizopatikana hivi karibuni zilitolewa kwa shirika hili; Shrika la ndege lenye huduma za daraja la kwanza, ubora kwenye huduma za chakula ndani ya ndege, ubora kwenye mandhari ya ndani ya ndege kwa ndege ya A380 iliyotolewa Julai 2016.

Kuhusu AirlineRatings.com
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 3013, AirlineRatings.com imekuwa ikijishughulisha kwenye ufuatiliaji wa ubora wa usalama na bidhaa kwenye ndege ulimwenguni. Hufuatilia hali ya usalama kupitia mfumo wake wa International Civil Aviation Organization (ICAO).

Tovuti hiyo imekuwa na wachangiaji milioni 14 huku wanaotembelea wakiwa ni wageni kutoka mataifa zaidi ya 232 ambao kwa makadirio wametembelea kurasa zaidi ya milioni 40. AirlineRatings.com inasherehekea mafanikio yake na kuhamasisha ufanisi kwenye sekta ya anga kwa kutoa tuzo za ubora za usafiri wa anga kwa ushirikiano wa timu ya wahariri.

Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika saba ambayo; Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi chini ya Etihad. 

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com
Shirika la Etihad lenye makao makuu yake Abu Dhab limejiwekea malengo ya kuhudumia abiria milioni 117 na kutoa huduma bora ya usafirishaji mizigo Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika.

Shirika lina ndege za Airbus na Boing 122, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa; ikiwamo 71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s na 10 Airbus A380s.