MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HABARI PICHA ZA UZINDUZI WA ALBUM YA SITASUMBUKA YA MWIMBAJI LIGHTNESS VINCENT NOVEMBA 13,NDANI YA KANISA LA MAISHA YA USHINDI ZIKO HAPA..

Jumapili ya jana Novemba 13 mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Lightness Vincent aliandika historia mpya katika kitabu cha huduma yake baada ya kuzindua DVD ya album yake ya pili inayokwenda kwa jina la Sitasumbuka.
Uzinduzi huo uliofanyika katika kanisa la Maisha ya Ushindi, Ubungo External ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam na kupambwa na waimbaji pamoja na wadau mbalimbali wa muziki wa Injili Tanzania.

Baadhi ya wadau na waimbaji waliokwepo katika uzinduzi huo ni pamoja na Mtangazaji wa kituo cha radio cha Praise Power,Boniphace Magupa ambaye ndiye alikuwa MC pamoja na mke wake Jessica BM ambaye ni mwimbaji na alihudumu,Mwimbaji na Mtangazaji Bishop Ben (Ben Bonge), Mtangazaji Innocent Mashauri na Hossein Gabriel wote kutoka Praise Power radio.

Wengine ni Happy Balolo,Emmanuel Choir, Silvanus Mumba,The Messengers Band , Kasaki Selemani pamoja na Bomby Johnson.

Baada ya Praise team kuongoza sifa na kuabudu, The Messengers Band walifungua kwa kuimba nyimbo mbili..

Zifutazo ni baadhi ya picha za matukio yaliyotokea kwenye tamasha hilo….

The messengers Band wakihudumu kwenye uzinduzi wa Lightness Vincent.


Baadhi ya watu waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Lightness Vincent

Meza ya Mgeni rasmi na wageni maalumu


Happy Balolo naye alikwepo kuhudumu


Mtangazaji Boniphace Magupa alikwepo kama MC wa katika uzinduzi huo.

Emmanuel Choir wakitumika.


Bishop Ben akifanya yake..


Janeth Jimmy akihudumu


Jessica wa Bm akilishambulia jukwaa


Hatimaye ukafika muda wa Lightness Vincent Kupanda jukwaani..

Risala kwa mgeni rasmi.


Baada ya Lightness Vincent kuimba wimbo wa kwanza uzinduzi wa album ukafuata.. 


Wachungaji wakiiweka wakfu album ya Sitasumbuka


Mgeni rasmi akikata utepe kwa niaba ya Alex Msama ishara ya kuizundua album hiyo


Baada ya Uzinduzi Lightness akapanda tena kuimba wimbo wa pili..


Baada ya Lightess Kushuka jukwaani Shughuli ikafungwa na waimbaji wengine akiwemo Kasaki Selemani na Silvanus Mumba.