RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HABARI : PROFESA NDALICHAKO AMESEMA ADHABU SHULENI ZISIHUSISHWE NA SIASA


Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako amesema siasa inatakiwa kuepukwa katika utoaji wa adhabu shuleni.

AKizungumza leo (Jummanne) wakati wa kufungua mdahalo wa wanafunzi wa sekondari mbalimbali za jiji la Dar-es-Salaam , Profesa Ndalichako amesema mwanafunzi anatakiwa kuadhibiwa baada ya bodi ya shule kujadili na kufanya maamuzi.

Waziri huyo amewataka wanafunzi kuwa makini kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii kwa sababu katika mitandao hiyo ya kijamii mijadala na picha zinazoikuka maadili ya nchi.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Binto Musa amesema tatizo kubwa linalosababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii ni kukosa uwezo wa kuchambua athari mbaya na nzuri zinazotokana na utandawazi.

Source : Mwanachi