RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HABARI : SERIKALI YAPINGWA MATUMIZI YA MISAADA YA TETEMEKO


Msimamo wa serikali wa kutumia michango iliyotolewa kwa aajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani kagera na kujungea miundombiinu umeendelea kupingwa huku baadhi ya wananchi na wanasiasa wakitaka suala hilo liangaliwe upya.

Diwani wa kashai (chadema) , Nuruhulda Kabaju akizungumza kwa kile alichokidai kuwa ndiyo maoni ya wananchi alisema wahisani walitoa misaada wakilenga kuwasaidia kwanza wananchi na suala la kujenga majengo ya serikali lingefua baadae

Kwa mujibu wa diwani huyo, kata hiyo imesajili nyumba 636 zilizobomoka na kaya 2556 kukosa makazi na kati ya hizo , shirika la World Vision Tanzania limetoa mifuko 212 ya saruji na nyumba 1300 ni hatari kuishi.

Source : Mwananchi