MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MAKONDA AWATAKA WAKUU WA WILAYA WOTE KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KISHERIA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku ya leo ni zamu ya wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni RC Makonda ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wamekuwa wanaitumia kinyume na utaratibu kwa kudhulumu haki za wanyonge ikiwemo kuuza viwanja kinyume na utaratibu, huku akisisitiza kuwa watendaji wa mtaa ndiyo inabidi wakae na mihuri hiyo.

Pia RC Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kuipeleka mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.

Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wanaitumia kinyume na utaratibu, leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na (kulia) ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro


.Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza machache na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akipokea ripoti ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwasili kwenye ukumbi wa Police Officer’s Mess akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo jijini Dar es Salaam.


Watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.