MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MASHALI AZIKWA NA MAMIA DAR


Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’.


Gari lenye mwili wa marehemu bondia,Thomas Mashali, likiingia katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.


Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa.


Jeneza baada ya kushushwa.


Waombolezaji wakiwa katika nyuso za huzuni wakati wasifu wa marehemu ukisomwa.


Kaka wa Mashali (katikati) akisoma wasifu wa marehemu.


Baba mzazi wa Thomas aitwaye Malifedha Christopher Mashali (mwenye fulana nyeupe kulia) akiwa katika majonzi.

Waombolezaji wakiendelea kupita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho.


Rais wa TPBO, Yasin Abdallah ‘Ostadh’ akitoa heshima za mwisho.


Mhariri kiongozi wa Gazeti la Championi, Saleh Ally (mwenye miwani) akitoa heshima za mwisho.


Dada wa marehemu aitwaye, Josephine akisaidiwa na ndugu wakati akipita mbele kuaga mwili wa kaka yake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akiwa amejumuika na waombolezaji katika maziko ya bondia Thomas Mashali kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Ndugu, jamaa na marafiki wakipita mbele ya jeneza.
Mazishi yakiendelea katika makaburi ya Kinondoni.


Mzee Mashali akiweka ua kwenye msalaba wa kaburi.Watoto wa marehemu wakiweka mashada katika kaburi la baba yao.Waombolezaji wakiwa makaburini wakati wa maziko.

HATIMAYE aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’ leo amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar akisindikizwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki.

Mbali na hao, Mashali aliyeuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita huko Kimara-Bonyokwa, Dar, amesindikizwa kwenye safari yake hiyo ya mwisho na wanasoka, akiwemo Athuman Idd ‘Chuji’, mabondia maarufu Tanzania, Francis Cheka, Mada Maugo, Francis Miyeyusho, Japhet Kaseba na bondia mkongwe, Rashid Matumla.

Akizungumza na Global Digital kwenye msiba huo, Cheka alisema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha Mashali ambaye kulikuwa na pambano kati yao lililokuwa linaandaliwa ambalo lilitarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu lakini hana budi kukubaliana na matokeo kwa sababu kila kitu kinapangwa na Mungu.

“Katika mapambano ya ngumi kwa upande wa uzito wa juu, kiukweli Tanzania imepoteza mtu muhimu sana. Mashali ameondoka wakati bado tasnia ya ngumi inamhitaji lakini ndiyo hivyo tena,” alisema Cheka.

Kwa upande wa meneja aliyefanya kazi kwa mara ya mwisho na Mashali, Sharifu Musili, alisema kuwa kifo cha Mashali kimetokea muda ambao hakuna aliyetarajia na kulikuwa na mipango mikubwa alikuwa anafanya juu ya bondia huyo.

“Tulikuwa tunafanya mipango Mashali akaishi nje ya nchi (Sweden au Ujerumani). Lakini kama haitoshi alikuwa na mapambano kadhaa ambayo alitakiwa kupambana. Moja lilikuwa tarehe 12, mwezi huu, lingine tarehe 26, mwezi huu na mengine mwezi unaofuata. Inasikitisha sana, nakosa hata maneno ya kuongeza,” alisema meneja huyo.

Mashali aliyeacha watoto saba, alizaliwa mwaka 1980, ameanza masuala ya ubondia mwanzoni mwa miaka ya 90 na hadi umauti unamkuta, alikuwa anamiliki mkanda wa dunia wa UBO. 
Mikanda mingine aliyowahi kushinda ni ya Ubingwa wa WBF Afrika, Ubingwa wa IBF Afrika, Ubingwa wa TPBO Tanzania na Ubingwa wa PST Tanzania.

Marehemu Mashali au Simba Asiyefugika kwa upande wa viwango vya mabondia wa ngumi za kulipwa Tanzania, alikuwa ni wa pili huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Cheka na ya tatu ikichukuliwa na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’.