MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

30.10.2016: MATUKIO YA TAMASHA LA MAOMBI LILILOFANYIKA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Siku ya Jumapili 30.10.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay, Mch. Francis Machichi, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Stanley Nnko na wainjilisti wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” waliweza kuongoza ibada ya maombezi iliyokuwa inafanyika katika kanisa hilo. 

Siku hiyo ilikuwa ni tamasha la maombi la kihistoria. Watu wengi waliweza kufunguliwa na kupokea miujiza yao, siku hiyo ilikuwa ni siku ya tofauti sana ukilinganisha na ibada zingine zilizofanyika katika kanisa hilo kwa sababu kulikuwa na nguvu za Mungu zilizo tanda kanisani hapo. Watu walitokwa na mapepo, majini, mikosi, laana n.k kwa kupitia maombezi hayo.
 

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa huruma zake alizozifanya kwa kuwatumia watumishi wake katika ibada hiyo. Mungu ni Mungu wa upendo kwani siku hiyo aliweza kugusa kila aliyefika katika kanisa hilo kwa njia azijuazo yeye. 
Pia tuna kila sababu ya kuwashukuru watumishi wa Mungu walioweza kutii sauti ya Mungu na kuwahudumia watu wenye uhitaji waliofika kanisani hapo wakiwa na mategemeo makubwa ya kupokea kile ambacho walikuwa wanakitegemea kukipata kutoka kwa Mungu.
 
Tunakukaribisha wewe ambaye hukubahatika kushiriki ibada hii ya tofauti siku ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Jinsi ya kufika kanisani ukifika kituo cha mabusi cha Makumbusho au Mwenge utakutana na mabusi utasikia kwa Mama kwa mama  hapo yatakufikisha hadi kanisani wote mnakaribishwa sana.