RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MGODI MAARUFU WA DHAHABU GEITA GGM WATOZWA FAINI YA SH. MILIONI 10 KWA KUKOSA CHOO CHA WAFANYAKAZI.

Mkurugeni mtendaji wa GGM wa pili kulia Bw. Terry Mulpeter akimuonyesha Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katikati, bwawa linalotumika kusambaza maji safi katika mji wa Geita.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Mungano na Mazingiraa Mhe. Luhaga Mpina akijiandaa kwenda sdehemu ya chini ya ardhi ya mgodi wa GGM 
Sehemu ya chini ya ardhi (underground) yenye dhahabu ya mgodi wa GGM inayosemekaka kukosa huduma ya choo kwa watumishi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya mia tatu, ikionekana kwa nje katika katika picha.
Bw. Simon Mushy Makamu wa Rais wa Mgodi wa GGM akijibu maswali ya Naibu Waziri Ofisi ya Maku wa Rais Mungano na Mazingira mhe Luhaga Mpina hayupo pichani kuhusu suala la mgodi kutiririsha maji ya mvua yaliyochanganyikana na sumu kutoka mgoni kwenda katika mazingira na maeneo ya vijiji jirani na Katoma
Sehemu ya kutupia na kutetekeza taka ngumu katika mgodi wa GGM Geita.
Mabwawa Ya majitaka la Mgodi wa dhabu wa Geita wa Geita Gold Mining maarufu kama GGM, ambapo imeelekezwa kuweka mtambo wa kusafisha Majitaka hayo kuingia katika mabwawa.


……………………………………………………………


Na Evelyn Mkokoi, Geita


Mgodi maarufu wa kuchimba dhahabu mjini Geita wa GGM umekumbana na adhabu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC katika Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Geita kwa kosa la kukosa vyoo vya wafanyakazi zaidi ya mia tatu (300) katika eneo la chini ya ardhi underground la uchimbaji wa madini ya dhahabu.


Hali hiyo imeipelekea NEMC kuutoza mgodi huo faini ya shilingi milioni 10, zinazotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne.


Katika ziara hiyo iliyomlazimu Naibu Waziri Mpina kuvaa vifaa maluum ili kuweza kuingia katika eneo la chini ya ardhi lenye mwamba mkubwa wa mgodi huo, akiambatana na baadhi ya maafisa aliongozana nao katika ziara yake, Naibu Waziri alijionea namna ambavyo eneo lenye idadi kuwa ya wafanyakazi kukosa huduma hiyo muhimu ya choo inayowapelekea kujisaidi vichakani na kuharibu mazingira.


Aidha Naibu Waziri Mpina Pia aliweza kujionea uharibifu mwingine unaofanywa na mgodi huo wa utiririshwaji wa Maji ya mvua yaliyochanganyikana na madawa hatarishi kwa mazingira na viumbe hai kwenda kwenye makazi ya wananchi.


Kufuatia hali hiyo, Naibu waziri Mpina alielekeza uongozi wa mgodi huo kujenga miundombinu rafiki kwa mazingira yatakayopelekea maji hayo kwenda katika mkondo sahihi..


Akiongea kwa Niaba ya GGM makamu wa Rais wa Mgodi huo Bw. Simon Mushy, alisema kuwa wapo kwenye mchakato wa kujenga miundombinu kwa kushiriana na Halmashauri ya Mji wa Geita.


Kwa upande wa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Katoma Bi. Magori James Katoka alisema kuwa vumbi na maji ya mvua vinavyotoka kwenye mgodi huo vimekuwa ni kero na changamoto ya muda mrefu katikma kijiji hicho.


Pamoja na malalamiko mengi ya wakazi wa Katoma Geita kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na mgodi wa GGM, Mgodi huo pia umefanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusambaza maji safi a salama katika mji wa Geita ukishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mkoa huo.



Ziara ya Naibu Waziri Mpina Katika Mkoa wa Geita ni muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira katika viwanda na migodi nchini.