RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SCORPION APANDISHWA TENA KIZIMBANI


DAR ES SALAAM: KWA mara ya nne leo, Salum Njwete ‘Scorpion’ ambaye anadaiwa kumtoboa macho Said Ally amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar na kesi yake kusogezwa mbele.

Askari magereza akiwa mbele akimuongoza Scorpion kuelekea chumba cha hakimu, Flora Haule.

Scorpion alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Flora Haule ambapo kesi yake ilitajwa na kupangiwa tarehe nyingine kutokana na upelelezi kutokamilika.

Askari akiwafukuza watu (hawako pichani) ili aweze kupita.

Kesi ya Scorpion ambayo inavuta hisia za watu wengi ambao wamekuwa wakijaa mahakamani hapo wakiwemo ndugu zake na wale wa upande wa pili wa Said, imepangwa kutajwa tena Novemba 16, mwaka huu.