RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TANZIA: MZEE HAMADI KILUVIA AFARIKI DUNIA, KUZIKWA JUMAMOSI USANGI


Familia ya Kiluvia inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpenzi Mzee Hamadi Kiluvia (pichani) kilichotokea jana alfajiri jijini Dar es salaam. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Regent Estate mtaa wa Migombani nyumba namba 72 ambapo ndipo ulipo msiba.

Msibani hapo ni hatua chache kutoka kituo cha mafuta cha Oil Com Victoria house, ila ili kufika unafuata barabara ya Mikocheni kwa Kairuki hadi njia panda ambapo unakata kulia na mbele tena unakutana na barabara inayotoka kwa JK ambapo unakata tena kulia. Hatua chache mbele utakuwa umefika.

Marehemu Mzee kiluvia atakumbukwa kama mmoja wa viongozi wa zamani serikalini na michezoni, ambapo katika uhai wake aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya, mmoja wa viongozi wa chama cha mpira wa miguu cha FAT enzi hizo pamoja na kuwa kiongozi aliyeheshimika sana katika klabu ya Yanga.

UPDATES: Mwili wa marehemu utapelekwa msikiti wa Regent Estate Ijumaa sita kamili mchana kwa ajili ya kuswaliwa baada ya swalat'Jumaa. Kisha utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mwisho kabla ya kuanza safari ya kupelekwa Usangi, Same, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi ambayo yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa saba mchana.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu baba yetu mahala pema peponi - Amin.

Matokeo ya Utafutaji