SHILO TANZANIA

SHILO TANZANIA

SHILO TANZANIA 2017

VIDEO: WASAMARIA WALIVYOMFUTA MACHOZI MWANAFUNZI WA UDSM ALIYELIA GAZETINI KWA KUKOSA MKOPO


Alionekana kwenye Magazeti likiwemo la Mwananchi akitokwa machozi na kujifuta baada ya kuona jina lake halipo kwenye orodha ya waliopata mkopo chuo kikuu cha Dar es salaam, jina lake ni Edson Mwakyombe ambaye alifaulu Form VI kwa Dividion 1.8

Baada ya Wasamaria kumuona kwenye gazeti, kupitia kwa Mwanasheria Albert Msandowakaomba kukutana nae tayari wakiwa wameguswa kumsaidia malipo na wakafanikiwa kulitimiza hilo November 1 2016.

Kiufupi ni kwamba Wasamaria wawili Isaria Mlaki na Andrew Komba waliojitokeza kumsaidia wamemuahidi kumsomesha kwa miaka miwili kila mmoja akimsomesha kwa mwaka mmoja.

Baada ya hayo Edson mwenyewe amesema ‘Nashukuru kwamba jambo hili limewagusa watu, naiomba serikali matatizo kama haya ya mkopo wayaangalie sana kwani kuna baadhi ya watu pia wanateseka sana huku chuoni kwetu, pia ninawaahidi hawa waliojitokeza kuwa nitahakikisha nafanya vizuri katika masomo yangu‘

Edson Mwakyombe akiwa na msamaria wake Isaria Mlaki aliyejitolea kumsomesha mwaka wa pili chuoni

Andrew Komba ambae ambae amejitolea kumsomesha masomo yake ya mwaka wa kwanza, Edson katikati na Mwanasheria Albert Msando

SHILOH TANZANIA 2017

SHILOH TANZANIA 2017