RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAZIRI NAPE AKATAA MAMLUKI SHIMMUTA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amekemea vikali baadhi ya tabia ya viongozi wa timu zinazoshiriki michezo mbalimbali kutumia wachezaji wasiostahili kutumika katika mashindano husika.


Ameyasema hayo wakati akizindua mashindano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Jijini Tanga ambayo yameshirikisha timu mbalimbali kutoka mashirika ya Umma na Binafsi Tanzania.


Mhe. Nnauye amewataka viongozi wa SHIMMUTA kufanya uhakiki upya wa wachezaji wa timu shiriki ili kuondoa lawama zinazoweza kutokea na kupata mshindi anayestahili kwa kufata Sheria na taratibu zote za mashindano.“Nawaomba viongozi muangalie na kupitia upya wachezaji wa timu shiriki ili kusiwe na zengwe lolote katika mashindano haya na mshindi katika kila mchezo apatikane kihalali” alisisitiza Mhe. Nnauye.


Aidha ametoa wito kwa mashirika kutenga muda na fedha ili kuwezesha timu zao kushiriki katika michezo ikiwa ni moja ya kujenga mshikamano na amani kwa watanzania na pia kujenga afya ya mwili na akili.Mashindano ya SHIMMUTA yameshirikisha mashirika ya Umma na Binafsi katika michezo 12 ikiwemo Mpira wa Miguu(Football), Mpira wa Pete(Netball),kuvuta kamba, Riadha, Mchezo wa vishale(Darts),Mchezo wa Pooltable, mchezo wa bao, Karata,kukimbia na magunia.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa mashindano ya SHIMMUTA wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Novemba 24, 2016 yanayofanyika Jijini Tanga.
Baadhi ya Timu zikiwasili katika katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Baadhi ya Timu zikiwasili katika katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bw. Hamis Mkalachi wakipokea maandamano ya timu shiriki zilizopokuwa zikiwasili katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akicheza muziki aina ya kwaito pamoja na wachezaji na viongozi wa timu shiriki wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu mbalimbali kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu mbalimbali kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akionesha ufundi wa kupiga danadana wakati wa uzinduzi rasmi wa wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga, akimshuhudia akipiga danadana hizo ni Mbunge wa Tanga Mjini Mhe.Musa Mbaruk.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM.