RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

04.12.2016: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA SHILOH TANZANIA 2016 NDANI YA KANISA LA MLIM WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mambo anayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" chini ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Siku ya kwanza ya Shiloh Tanzania 2016 iliyofanyika siku ya Jumapili 04.12.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu wengi sana walijitokeza madhabahuni kuyakabidhi maisha yao mikononi mwa Yesu ili yawe salama hapa duniani na huko mbinguni. Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Stanley Nnko, Mzee wa kanisa Mzee Major Malya, Mch. Prisca na Mch. Francis Machichi waliweza kuwaongoza sala ya toba na baadae kuwaombea. Baada ya maombezi walishiriki ibada kuu na hatimaye walibatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumanne wiki hii wataaanza masomo yao ya kukulia wokovu.

Tunakukaribisha na wewe kuja kwa Yesu ili uishi maisha ya kumpendeza Mungu. Umeitumikia sana dunia, sasa anza maisha mapya na Yesu ili uwe na amani na uhakika wa kufika mbinguni. Ibada za Jumapili huanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Ila kipindi hiki cha Shiloh kwa siku 8 za Moto usiozimika kipindi cha maombezi ni saa 4 aubuhi hadi saa 8 mchana na Ibada ya Shiloh ni saa 9 mchana hadi saa 12 jioni. Mungu akutie moyo kipindi hiki cha Shiloh kilicho na upako kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake, Bishop Danstan Maboya, Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini, Mch. Noah Lukumay, Mch. Komba, Mch. Francis Machichi na wachungaji wote wa makanisa ya Mlima wa Moto Tanzania nzima































 TANZANIA 2016 TANZANIA 2016