RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

04.12.2016: BISHOP DUNSTAN MABOYA AHUBIRI JUU YA WATU KUFANYA KAZI NA KUSTIKUWA TEGEMEZI KATIKA KUSANYIKO LA SHILOH TANZANIA 2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

JITAHIDI KUYASHINDA MAJARIBU
Bishop Dunstan Maboya alichokihubiri  siku ya Jumapili 04.12.2016,  kusanyiko la Shiloh Tanzania lililofanyika katika kanisa la Mliama wa Moto Mikocheni “B” alikuwa na haya ya  kusema,  Mtu akiona maisha yake yameanza kuwa shwari, hapo kinaanza kuja kiburi. Nilikutana na rafiki yangu  nchi za nje nikamkuta na vitu vya ajabu ajabu, akasema, “Unafahamu hapa U.S mambo ni mengi, na haya mambo ya U.S tuyaachie hapa hapa”, nikasema, “Hapana  Mungu wa U.S ndo Mungu wa Tanzania yeye habadiliki.” rafiki yangu huyu alitaka kuniingiza choo cha kike mwanangu, ili niende tofauti na taratibu za Mungu, nikashtuka mwanangu, nikasema hili jaribu ninaliruka mpaka ashangae. 
Majaribu hayafanani, inapofika kipindi cha majaribu na kupimwa imani yako  inakupasa kusimama imara. Mungu anataka kukuweka uwe “Top” hata kama utakuwa wa mwisho anataka kukubadilisha kuwa wa kwanza,  kukuinua, kukupa afya njema, ujenge nyumba yako na uozeshe watoto wako na mafanikio mbalimbali. Katika maisha ni azima ushiriki matatizo kwani yanakusaidia kupasua kichwa chako na kufikiria makubwa. 
Jaribu lipokuujia ni lazima uwe makini sana jinsi ya kulikwepa mwanangu. Watu wengi sana na hasa vijana wametumbukia katika mtego wa shetani na wanashindwa kutambua majaribu wanayopitia, kila kitu kwao wanaona sawa tu, na hii ni kutokana na kutokuwa na ile hofu ya Mungu, na kukosa Roho Mtakatifu atakaye waongoza katika kutambua jema na baya. Kwahiyo muombea sana Mungu akusaidie kutambua majaribu yako, usije ukatumbukia humo.

HUSIKA NA MAISHA YA MWANAO
“Ukisoma Yeremia 29:4 Bwana wa majeshi, Mungu wa Israel awaambia hivi watu wote waliochukuliwa mateka, waliofanya wachukuliwe toka Yerusalemu mpaka Babeli, “Jengeni nyumba mkakae ndani yake, mkapande bustani, mkale matunda yake. 
Oeni wake mkazae wana na binti, kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti mkaongezeke huko wala msipungue.” Kwanza kabisa umeambiwa kajenge nyumba siyo kusubiri wazazi wako wafe ndipo urithi nyumba zao,  ndio maana siku hizi kesi za urithi ni nyingi, mirathi ndugu mpaka wanagombana. 
Achana na nyumba ya urithi jenga yako.  Ibrahimu alikaa akatulia akamwambia kijakazi wake, “Nenda kwa kijiji cha mama yangu ukamtwalie mwanangu mume.” Hapo alitumia akili na yule kijakazi nae akawa anaenda akisema, “Mungu naomba unisaidie nisimkosee bwana wangu.” Unapokuwa kwenye maombi yako, mama angalia binti yako anacheza wapi lazima akili yako ifanye kazi. 

Mungu anakusaidia wewe, Mungu anakwenda kukuinua lazima uhusike na maisha ya watoto wako, na huwezi ukawa na nguvu ya kutoa elekezi kwa wanao kama uchumi wako uko ovyo lazima uchumi wako uwe “stable” na unapotoa sauti kwa wanao nao wanatii kwasababu una mshiko mwanangu, usipokuwa na mshiko watakudharau hao wanao. Namuomba Mungu katika Shiloh hii Bwana akupe mambo makubwa.”


SIRI YA KUINULIWA  LAZIMA UWE NA MAADUI
Utakuta Mtu anakuwa kwenye chumba cha mtihani na  mtihani huo ni wa kufanya  muda wa dakika 45, eti unapiga kwa dakika10 mwanangu hiyo ni ujinga utakosea. Wasomi washasema ni wa dakika 45, kaa tulia kwenye chumba cha mtiahan,  kutoka mapema kwenye chumba cha mtiahani siyo sifa. Unatangaza kujiua wakati Mungu anasema, “Mimi ni Mungu nipo nae,  naelewa hatima yake na sitakuacha wala sitakupungukia na uzao wa tumbo lako mimi nitaubarika”,  halafu wewe unasema, “Heri nife”Je, ukifa utaenda wapi?
 Mungu ana makusudi, Yusufu alikuwa amemuelewa vizuri Mungu, ukisoma Mwanzo 37, Yusuph alimpenda sana Mungu, akazungumza mambo yake wazi wazi kila kitu akaweka wazi, na mara nyingi watu wawazi wanaonekana hawana akili, siyo hawana akili bali wanamjua Mungu wanaomwabudu. Yusuph alikuwa muwazi hakuwa mchoyo wa ku “share” mawazo yake, alikuwa mtumishi kwa watu wengine, akawaeleza ndugu zake, ndugu zake mambo fulani lakini wakachukia.
Wewe unalalamika siku hizi eti kuna majirani wanakuchukia si afadhari majirani, wakati Yusufu alichukiwa na watu wa kiuno kimoja. Wewe huna vita kubwa na wanaokuchukia kwa sababu matatizo ya jirani unaweza ukatatua na ukabadilisha njia, lakini Yusufu alichukiwa na  watu wa nyumba moja, watoto wa baba mmoja wamemchukia. Sisi tunapenda sana kwenda juu lakini hatutaki kuinuliwa,  na siri moja ya kwenda juu lazima uwe na maadui.

SHIKA SHERIA ZA MUNGU ILI UFANIKIWE KIMAISHA
Watu wanaokuonea wivu hiyo ndio siri kubwa ya kwanza lazima uwe na watu watakao kuonea wivu. watu wataweka kizuio mbele yako, watu watakuchafua kwenye magazeti, lakini utang;ara tu. Je, hamjifunzi kwa mama yenu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare? 
Hiyo ni siri moja kubwa lazima upate. Watu wanaokuchukia, Mungu anasema, “Nitakubariki mbele ya macho ya adui zako”. Kumbukumbu la Tolati 28:13 linasema, “Wewe siku zote utakuwa juu, utakuwa kichwa na wala hutashuka chini lakini kwa kushika sheria zangu”. Usiseme nimeomba sana kwa Mungu, lakini je umeshika sheria anazokuagiza Mungu uzishike? Tuache ya 1,2,3 najua unaweza nazungumzia ya 7,8,9 na 10 unaiweza? 
Hiyo ya kwanza unaielewa ndiyo imekupa hata cheo kanisani, nazungumzia 8,9 na 10 hizo ndo zinakuchakatua mwanangu. Katika Shiloh hii Bwana akafanye uaminifu kwako..pokeeeeaaa. Huwezi ukabaki juu kama utashindwa kushika sheria za Mungu. 
Mungu akamwambia, “Kondoo wangu ukashike sheria bila kuangalia kushoto wala kulia ukatende sawa sawa ndipo utakapofanikiwa”. Kanuni hazijabadilika, kanuni zipo palepale. Je, upendo wako kwa Mungu anautambua? Jaribu kutulia sehem fulani na ukashike sheria za Mungu utakapo zikamata sheria jinsi inavyopasa kuwa utayaona mafanikio tu.

FAIDA ZA KUTOA FUNGU LA KUMI KWA MTU YEYOTE YULE
Kuna mtumishi wa Mungu katika mahubiri yake aligusia fungu la kumi na mimi nikasema ngoja nipige gia kanuni za fungu la kumi anasema leteni zaka kamili hekaruni mwa Mungu. Tunao watumishi wengi ambao Mungu anawatumia vizuri na wanamuwakilisha Mungu lakini ukifika wakati wa kutoa fungu la kumi wanakwepa, lakini mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na kwamba alianza kazi amekuwa akikua siku baada ya siku na amekuwa mwaminifu katika suala la utoaji. 
Kuna usemi unasema, ”Utawatambua kwa matunda yao”, Mungu akampa neema ya kufungua huduma ya makanisa na hayo makanisa amewapa wachungaji. Na hiki kitendo siyo kitu rahisi. Kuna baadhi ya watumishi  wanaweza kuhangaika kwa miaka 20 lakini  akawa na watu 200 tu, na hii inaweza kuchangiwa na watu kutotambua kutoa fungu la kumi. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alivyotambuafaida za kutoa fungu la kumi, Mungu akampa neema ya kuwa na watu wengi na kufungua makanisa mengi kama Tabata, Kigamoni, Bunju, Dodoma n.k. 
Ukitaka kufanikiwa kwa kila jambo ni lazima uwe mtoaji wa fungu la kumi na uwe muombaji mbele za Mungu. Ukifanya hayo utaona mambo yako yanaiva mwanangu.



SIRI YA KWENDA JUU KIMAISHA
Kwa utulivu wa Mungu uliondani yangu. nikupe siri ya kwenda juu kimaisha. Nadhani unajua kuwa mbingu na nchi zitapita lakini Neno lake Mungu litasimama na Mungu anasema, “Neno langu halitanirudia bure” na ndiyo maana watumishi wa Mungu wanasema, “Ni wakati wakuangalia Neno linasema nini?”. 
Namuomba Mungu katika Shiloh Tanzania hii,  “Moyo wako ukasimame na Mungu”, Yesu alisema’ “Moyo u hai lakini mwili ni dhaifu” lakini hakuwahi kushindwa, maombi yalisimama pale pale na mwisho wa yote akaona haieleweki akasema, “Mapenzi yako yatimizwe”. 
Namuona Bwana anakwenda kukufanikisha siku ya leo na hizi siku zilizobaki za kuhitimishwa kwa Shiloh, Mungu akafanye jambo lolote juu yako, Bwana anaweza akaweke tandalao katika maisha yako. Ukitaka kufanikiwa kimaisha zingatia kutoa fungu la kumi, kutoa zaka, kusoma Neno la Mungu na kuyaishi yale uliyosoma, kuwa na upendo kwa watu wote, kusaidia wenye uhitaji, kutii sauti ya watumishi wako, kujishusha kwa utukufuwa Mungu, kufanya kazi kwa bidii kwa kumshirikisha Mungu, kufanya biashara halali, kuyaheshimu mapato yako, kuwa mbunifu katika kazi yako, kuomba na kufunga na mengine kama hayo


UWE MACHO NA WATU WANAOKUTABIRIA
Natakaka nikuambie kuwa, Nabii hana kibali cha kula zaka. Hivi ndivyo alivyoanza kuzungumza. Leta zaka madhabahuni” Mungu anaangalia ni jinsi gani unamheshimu, unavyoheshimu madhabahu, na ni lazima kitu kitokee kwa kuiheshimu madahabahu. 
Mungu atusaidie, watumishi tuko wengi tuna maneno matamu sana lakini hatuna upako na watu wanaumizwa na huduma zetu, watumishi tunawatabiria watu mpaka tunawapa pressure na kuwachanganya tunaowatabiria. Ninaomba sana manabii wanavyotabiri wajaribu kusikiliza Roho wa Mungu na sio kuleta maneno matamu ili watu waaamini na na kuwatumikia katika makanisa yao. Mungu sio wa mchezo mwanangu, Mungu anahitaji watumishi wake wasioleta maneno matamu matamu kuwalainisha waumini wao. Mungu anataka Neno la kweli kutoka kwenye Biblia. 
Mbwembwe nyingi hazisaidii katika ufalme wa MUNGU. Mungu na atusaidie sana katika kipindi hiki vcha manabii wengi ambao hawajaitwa na Mungu. Kama wewe ni Nabii jiulize unabii wako ni kutoka kwa Mungu au unatumia akili zako kuwalagai watu? Tusiwachanganye watoto wa Mungu na kuwatisha kwa kuwatabiria vitu ambavyo havipo katika maisha yao.

UNAMHITAJI MTU ANAYEKUSEMA VIBAYA
Katika maisha yako unamhitaji mtu anayekupa changamoto za kimaisha, ukiona ndugu yako anakutesa eti kwasababu unaishi kwake, wewe mpende kwani anakufundisha jambo litakalokusaidia katika maisha yako ya kujitegemea. 
Hayo maudhi ni daraja la kwenda kwenye maendeleo yako ndio maana upo mahali hapa. Waswahili wanasema, “Jirani akikunyima chumvi usimchukie amekufundisha kuweka akiba” unamwitaji Yuda ambaye atasimama na kukupa scholarship. 
Kuna watu waliingia hapa mjini kama ma “housegirl” lakini leo wanaendesha TOYOTA. Wewe kama ulitelekezwa kijijini ukaonekana huna maana lakini leo una maana, ulizarauliwa katika utoto wako lakini leo unaheshimika, usiogope maudhi, hakuna kukimbia kwa sababu Mungu aliyajua maisha yako. 
Unamwitaja Ishumahili ambaye atakununua na kukupa “scholarship”, unahitaji mtu anayekusema maana huyo anakufungulia njia ya mafanikio na kupanua akili yako ya kufikiria kujiweka huru na mateso unayopitia. Katika Shiloh hii Mungu akupe moyo msafi. Wapo watu wamekaa kwenye wokovu au utumisha muda mrefu wanakuja kufanya makosa ya kidini kwa sababu imani yao lazima ipigwe vita. 
Mungu lazima apime kwanza imani yako katika mafanikio aliyotupa, tusimtukane Jehova kwasababu tunapitia magumu na kusemangwa na ndugu zetu au jamaa zetu. Yusuph imani yake ikaja kujaribiwa akayumba, kwenye dhiki na kwenye shida unakuta siyo rahisi kupita kwenye majaribu kwa sababu shida ni ule utata wenyewe sasa wapendwa hata pepo akiwepo huwezi jua kama yupo pepo, unakuja kuona anakuvamia tu. Jitahidi kuwa mvumilivu sana.

ACHA KUNUNG’UNIKA ETI NDUGU HAKUSAIDII

Usimchukie ndugu yako kama amekutimua nyumbani kwake na ukaondoka  na mabegi yako, hali ngumu ya kimaisha imesababisha wakutimue, na pengine  walipanga kukuua. Leo kuna wengine wako kwa ndugu zao wanakula na kulala bure lakini wanaanza kusema, “Ndugu yangu mbaya, hanipi hela ya matumizi”. 
Wewe unaafadhali kwani kuna wengine  walipangiwa kifo na ndugu zao eti kwasababu wanakaa nyumbani kwao na kuwa tegemezi kwa kila kitu, acha kunung’unika hupati pesa na matumizi ila chakula na malazi unapata bure. Mtindo wa kunung’unika uache kuanzia leo. 
Biblia inasema, “Wakasemezana wao kwa wao, tazama yule bwana anakuja twende tukamuue na kumtupa katika birika moja,  japo nasi tutasema, mnyama mkali amemla tutaona zitakuwaje ndoto zao? Rubeni akasikia akamuokoa katika mikono yao, akasema, tusimuue, tusimwage damu katika birika hii lililopo nyikani”. 
Hapa wote walikuwa katika kundi moja linalotaka kumuua lakini alitokea Rubeni yaani hakupendi lakini hataki ufe, anakuchukia kabisa lakini hataki ufe. Leo hii ndugu yako uko nae hapa mjini baada ya kuwa nae hapa mjini, umekaa nae vizuri unakula chakula anaanza kukusema ovyo, “Unakaa tu hapa mjini ondoka pamekushinda”. Ukiona mtu wa aina hii  hakupendi lakini amekupa chakula, hataki ufe basi hutakiwi kuumia moyo  ipo siku yako utatoboa, utakuja kukutana na mtu ambaye ndiye atakuwa tumaini lako.