MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

04.12.2016: BISHOP DUNSTAN MABOYA ALIVYOWASILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KWAAJILI YA SHILOH

Bishop Dunstan Maboya kutoka Arusha Tanzania akiwasili ndani ya nyumba ya Bwana ya Mlima wa Moto Mikocheni “B”pamoja na Mch. Madoshi  tayari kwa kazi ya Bwana siku ya Jumapili 04.12.2016. Ibada hii ilihudhuriwa na watu wengi kutoka kila pande zote za Tanzania. Hii ikiwa ni siku ya kwanza ya uzinduzi wa SHILOH Tanzania 2016 ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka. Mwaka huu 2016 Shiloh Tanzania itachukua siku 8 za Moto Usiozimika ndani ya kanisa la Moto Mikocheni “B” na kuhitimishwa siku ya Jumapili 11.12.2016.

Watumishi wa Mungu kama Bishop Dunstan Maboya, Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini, Mch. Noah Lukumay, Mch. Madoshi, Mch. Kimba kutoka Dodoma, Mch. Sebastian, Mch. Stanley Nnko, Mch. Prisca, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Simtovu, Mch. Wambura,  na wengine wengi watakuombea katika kongamano hili la kimataifa.

Pia kutakuwa na waimbaji kama Happy Kwaya, Joybringers, Masanja, Christina Shusho na Bahati Bukuku, nao watashua uwepo wa Mungu ambao utafanyika Baraka kwako.

Kama wewe unasumbuliwa na kansa, UKIMWI, kifua kikuu, Vidonda vya tumbo, TB, Kisukari na magonjwa mengine yote Yesu anakwenda kuyaponya kupitia watumishi wa Mungu. Pia kama unapitia mapito kama kukosa ada, uchumba, kutopata watoto, madeni sugu, kufukuzwa kazi, Umaskini na kila shida, kila matatizo Bwana atakusaidia, wewe amini tu kuwa kila kitu kwa Mungu kinawezekana ukiomba na kutii maagizo yake.

 Mch. Madoshi (kushoto)

 Bishop Dunstan Maboya akishuka katika gari lake ara baada ya kuwasili kanisani hapo