MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

04.12.2016: MCH. ELIZABETH LUCAS AKIFUNDISHA KATIKA KIPINDI CHA SUNDAY SCHOOL SIKU YA JUMAPILI YA SHILOH TANZANIA 2016 NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mch. Elizabeth Lucas siku ya uzinduzi wa Shiloh Tanzania 2016 tarehe 04.12.2016 aliweza kufundishe Neno la Mungu katika kipindi cha Sunday School. Kupitia mafundisho yake yenye upako wa aina yake, watu wengi walionekana kuguswa na ujumbe wa Mungu.

Kumbuka hii ilikuwa ni siku ya kwanza kwa Mwaka 2016 kufanyika kongamano kubwa la Shiloh ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Mwaka huu litachukua siku nane kuanzia 04.12.2016 hadi 11.12.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani siku hii ya Jumapili watu walibarakiwa sana na mafundisho ya Mungu kutoka kwa watumishi wa Mungu aliowateua kwa kazi yake.

Hujachelewa na wewe kushiriki baraka hizi, kwani Shiloh hii itachukua siku 8 na hivi sasa zimebaki siku 7. Ibada ya maombezi inaanza saa 4 asubuhi hadi 8 mchana na saa 9 mchana nhadi 12 jioni ni Ibada ya Shiloh ambapo Bishop Danstan Maboya, Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini, Mch. Noah Lukumay, Mch. Komba, Mch. Francis Machichi, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Sebastian, Mch. Stanley Nnko na wengine wengi watakuwepo.

Usikose baraka hizi za Mungu. Mungu akubariki sana