MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

04.12.2016: REV. ELIAS NDEDA KUTOKA AFRIKA KUSINI KATIKA SHILOH TANZANIA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SISITIZA WATU KUFANYA KAZI KWA BIDII


Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini kwa mara ya kwanza tangia Shiloh ianze Jumapili  04.12.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, siku ya Jumatano 08.12.2016 akiongea na waumini wa kanisa hilo alisema katika siku hizi 3 zilizobaki za kuhudumia watu mbalimbali katika Shiloh hii atajikita sana katika  kufundisha juu ya kujikomboa na umaskini na kuachia upako wa   utajiri kama yeye alivyobarikiwa na Mungu na kuwa miongoni mwa watu ambao wamejikomboa kiuchumi. Alisisitiza sana kuhusiana na kukerwa na umaskini unaotesa sana watoto wa `Mungu na kujikuta wanaingia katika dhambi. Rev. Ndeda alipenda kuona watu wakiwa na furaha na wakifurahia wokovu wao na kuwa mabalozi wa Yesu wasio na njaa. Pia atafundisha Neno la Mungu na kukukombea ili uwe huru katika vifungo vya shetani ambavyo vinawatesa walio wengi.

Kwahiyo jitahidi sana kwa siku hizi tatu ushiriki ibada hii ya Shiloh, na ratiba yake  ni kana ifuatavyo: Maombezi ni saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana na Ibada Kuu ya Shiloh ni saa 9 mchana hadi 12 jioni. Mungu akubariki sana.