RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

05.12.2016: BISHOP DR. DUNSTAN MABOYA NA BISHOP DR. GERTRUDE SIKU YA PILI YA SHILOH TANZANIA INAYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WALIWEZA KUWAOMBEA WATU WENYE MAGONJWA SUGU TU


Bishop Dr. Dunstan Maboya baada ya kuhubiri siku ya Jumatatu 05.12.2016 katika kusanyiko la watu wa Mungu la SHILOH linaloendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare hadi Jumapili 11.12.2016 aliweza kupata muda wa kuwaombea watu wenye magonjwa sugu na baadhi yao walipokea uponyaji wao hapo kwa hapo. Kuna baadhi yao walipona kansa, kutosikia, kutoona vizuri, uvimbe katika miili yao. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumtumia mtumishi wake kutatatua matatizo yetu kwa damu ya Yesu.
Nikukaribishe katika kipindi cha maombezi kwa siku hizi chache zilizobaki kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana na Ibada kuu ya Shiloh ni saa 9 mchana hadi saa 12 jioni.