RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.12.2016: BAADHI YA WACHUNGAJI KUTOKA MIKOA 24 WALIOSHIRIKI SHILOH TANZANIA WALIWEZA KUWASALIMIA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMATANO

Mch. Fungo kutoka Mwanza na wachungaji mbalimbali siku ya Jumatano 06.12.2016 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kutoa salamu zao kwa waumini wa kanisa hilo na kuwatakia Shiloh njema kwa kipindi cha siku 8 za Moto Usiozimika. Shiloh ilizunduliwa siku ya Jumapili 04.12.2016 na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na Bishop Dr. Dunstan Maboya kutoka Arusha Tanzania. Pia kuliwa na watumishi wa Mungu kutoka katika mikoa 24 ya Tanzania kama vile Mch. Komba, Mch. Fungo, Mch. Simtomvu, Mch. Wambura, Mch. Sebastian, Mch. Karisto Kyando, Mch. Dickson, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Stanley Nnko, Mch. Noah Lukumay, Mch. Francis machichi na wengine wengi.

Pia kulikuwa na waimbaji wa kimataifa kama vile Masanja, Christina Shusho , Bahati Bukuku Kwaya ya Joybringers na Happy Kwaya za Mlima wa Moto Mikocheni na Kwaya kutoka Mlima wa Moto Dodoma kwa Mch. Komba.


Sasa unakaribishwa wewe unahitaji Mungu aongee na wewe katika maisha yako. Kuna jambo ambalo ungependa Bwana akutendee kupitia Shiloh hii na limekuwa likikusumbua kwa muda mrefu sasa. nakuambia kupitia Shiloh hii Bwana wa huruma na upendo atakwenda kukuponya kama utatubu na kuamini kuwa Mungu yupo na anaweza kukutendea. Imani yako na juhudi za kumtafuta Mungu ndizo zitakufanya wewe upokee majibu yako na baraka zako kutoka kwa Jehovah.


Kama utakuja kanisani ukiwa na hofu na huna imani kuwa Bwana atakufanyia jambo kupitia watumishi wake, nataka kukuambia kuwa utatoka kanisani ukiwa mzigo wako umeubeba. waamini watumishi wa Mungu kwani wao wamebeba ujumbe wako kutoka kwa Mungu. Tii sauti ya Bwana kupitia kinywa cha watumishi wa Mungu.

Anza kutenda mambo mema yatakayokufanya uwe karibu na uwepo wa Mungu kila wakati wote. Soma Biblia kwani huko kuna maagizo yote ya Mungu ambayo mwanadamu anatakiwa kuyafanya. Sikiliza nyimbo za dini zitakuinua Kiroho na fanya kazi kwa bidii bila kusahau kushiriki kazi za kanisani. Jitahidi kuwa mtoaji kanisani na Mungu hata kuacha kamwe. Mungu akubariki sana