MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

07.12.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWATAKA WATU KUTUMIA MAMLAKA DHIDI YA MAADUI ZAKE NA KUWAPOFUA MAADUI KATIKA IBADA YA IJUMAA YA SHILOH

Ni wakati mzuri wa kukalabati kiroho chako, ni wakati mzuri wa kutubu na kuanza upya katika Bwana. Ulishindwa kwa miezi 11, mwambie Mungu, “Nipe nguvu mpya ninapoingia mwaka mpya wa 2017 niwe mtu mwingine.” Nilikuwa nasoma a 2Wafalme 6: 20 pale tunaona mtumishi wa Mungu alikuwa ameitwa na Mfalme, alipoona amekawia akatuma wanajesha, mafarasi na magari aende akakamatwe; mtumishi wa Mungu alivyotoka nje alivyoona umati wa watu akasema, “tufyile”, maana yake ilikuwa inatisha akasema, “Sijui tujifiche wapi?” Akasema, “Usijali”, akamgusa macho yake akamwambia, “Unaona nini?” akasema, “Ninaona walio upande wetu ni wengi kuliko hilo kundi lakini kitu ambacho kinanifurahisha, nguvu iliyo ndani ya mtu wa Mungu.” 

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Yule baba akasema, “Na wawe vipofu, uwapofue macho wote wasione”, ghafla waka vipofu mara moja kwa Neno la mtumishi wa Mungu akasema, “Haya mnifuate mnayemtafuta, mimi najua alipo”, akawapeleka mpaka samalia walikotoka. Unayo mamlaka ya kuwapiga vipofu adui zako aliwapiga upofu mpaka walivyofika. Bwana akasema, “Imekuwaje huyu mtu wanashindwa?.” Jisomee Kutoka 10, Musa alisema, “Nyoosha mkono wako elekea kwa Wamisri”, kukawa na giza nene wakawa wanabaki kupapasa papasa. Adui zako lazima uwapofue macho wambie mji kama huu wasinione kwa vioo vyao vya kichawi, wasinione kwa Tv zao za kichawi, uwapofue macho wasinione, kwa jina la Yesu.
Kutoka kulia ni Bishop Dr. Dunstan Maboya, Mch. Noah Lukumay na Mch. Francis Machichi

Unayo mamlaka, tumia mamlaka uliyo nayo maadui zako watasambalatika. Ayestahili heshima mpeni heshima, anayekushambulia na wewe mshambulie kwa maombi. Wote tunasafari moja ya kwenda mbinguni kwahiyo ukiomna adui analeta kauzibe basi kazibui ili upenye ufike mbinguni. 


Kila mtu anapitia “challenges” nyingi katika maisha, ikiwa pia ni pamoja na hawa maadui zetu wanavyojitahidi kuvuruga “future” yako. “Challenge” zipo tu. Unatakiwa kuwa kidume wa kupambana na changamoto za dunia, usiwe mtu wa kukata tamaa unapoona gumu liko mbele yako. 
Ishi kama simba, usiwe mwogo kwa majaribu unayopitia kwani kupitia majaribu hayo akili yako inapanuka na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiria makubwa na jinsi ya kujikwamua katika majaribu yako. Unaposhinda jaribu lako hapo ndipo unagundua kuwa Mungu anaweza yote na unaposhindwa kuvuka jaribu lako bado Mungu ni mshindi tu kwasababu yeye amekuandalia kesho yako ya kulitatua jaribu lako.